Home BUSINESS WAZIRI UMMY ATETA NA BOSS MPYA WA VODACOM TANZANIA

WAZIRI UMMY ATETA NA BOSS MPYA WA VODACOM TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo amekutana na Mkurugenzi Mpya wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bw. Philip Besumire kwa lengo la kujitambulisha na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya Afya.

Miongoni mwa mambo waliyojadilina ni pamoja na Kampuni hiyo ya simu kuendelea kushirikiana na Wizara ya Afya hasa katika kipindi hiki cha tishio la Ebola kwa kutoa jumbe mbalimbali kwa siku ili kuwaelimisha wananchi.

Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma na kimewakutanisha viongozi wa Wizara akiwemo Mkurugenzi wa huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Dkt. Ahmadi Makuwani na Viongozi wengine kutoka Vodacom Tanzania.

Ugonjwa wa Ebola ulioripotiwa kutokea nchi ya jirani ya Uganda, ambapo hadi sasa Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa elimu pamoja na utayari katika mipaka yote ya nchi kwa kutoa elimu na uchunguzi wa kina dhidi ya Ugonjwa huo.

Mwisho.

Previous articleHabari picha: ZIARA YA NAIBU MEYA OJAMBI MASABURI PUGU
Next articleSERIKALI YAENDELEA KUJIIMARISHA KATIKA UDHIBITI WA UGONJWA WA EBOLA USIINGIE NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here