Home BUSINESS WAZIRI BALOZI PINDI CHANA AKUTANA NA KAMATI YA KITAIFA YA MAANDALIZI YA...

WAZIRI BALOZI PINDI CHANA AKUTANA NA KAMATI YA KITAIFA YA MAANDALIZI YA ONESHO LA UTALII LA KIMATAIFA LA S!TE

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Onesho la utalii la Kimataifa linalojulika kama “Swahili International Tourism Expo (SITE)” kwa lengo la kupata taarifa ya maandilizi yanayofanywa na kamati hiyo. Onesho hilo la Utalii linatarajia kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City uliopo jijini Dar es Salaam tarehe 21 hadi 23 Oktoba, 2022.

Akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo, Balozi Dkt. Pindi Chana amewasisitizia wajitume na kuhakikisha onesho hilo linafanyika kwa kiwango cha kimataifa.

“Nategemea kuona taasisi zote za Wizara ya Maliasili zinahamasisha wadau wao kushiriki katika onesho hili na kutumia fursa hii kufanya biashara na wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali duniani waliothibitisha kushiriki katika onesho la mwaka huu”.

Amesema Serikali imedhamiria kuwanyanyua wafanyabiashara za utali wa Tanzania kwa kuendelea kuandaa onesho la sita ambalo linaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassani za kuanzisha programu ya The Royal Tour Tanzania inayotangaza utalii wa Tanzania.

Ameongeza kuwa Kamati hiyo imepewa dhamana na kuaminiwa, hivyo lazima kila mjumbe apambane na kuhakikisha anatekeleza jukumu alilopangiwa.

Amebainisha kuwa kamati hiyo imeshirikisha taasisi zote muhimu ambazo zina mchango mkubwa wa kufanikisha Site 2022.

Onesho la kwanza la Swahili International Tourism Expo lilifanyika mwaka 2014 katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here