Home BUSINESS WAWEZESHENI WANAWAKE WAJIUNGE KWENYE JUKWAA LA KUWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI

WAWEZESHENI WANAWAKE WAJIUNGE KWENYE JUKWAA LA KUWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI

Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, Dkt. Doroth Gwajima ameziagiza Halmashauri zote nchini zihakikishe zinawawezesha wanawake kujiunga na jukwaa la kuwainua wanawake kiuchumi ili kuchechemua uchumi wao kupitia fursa zitokanazo na jukwaa hilo.

Maadhimisho ya siku ya mwanamke anayeishi kijijini yanafanyika kwa mara tano nchini ambapo yalipitishwa kwa azimio namba 62 la mkutano mkuu wa umoja wa mataifa tarehe 18 disemba 2007 na kutambuliwa na mkutano mkuu wa nchi wanachama wa umoja wa mataifa na kuadhimishwa kwa mra ya kwanza duniani 15 octoba mwaka 2008.

Waziri Dkt. Gwajima ametoa agizo hilo akiwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Mkoani Morogoro kwenye kilele cha siku ya kimataifa ya Mwanamke anayeishi kijijini ambapo kitaifa yamefanyika Mkoani humo.

Alisema kupitia jukwaa hilo wanawake wanaweza kuweka ajenda za kiuchumi na kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake hasa zile za ukatili wa kijinsia ambazo zimekuwa chanzo cha wanawake wa kijijini kuishi maisha duni.

“Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan alionyesha wazi nia yake ya kuwasaidia wanawake kiuchumi ndio maana aliaanzisha jukwaa hili ili wanawake wajikwamue kiuchum.” Alisema Waziri Gwajima.

“Kutokana na nia ya Mhe. Rais nizitake Halmashauri zote kupitia kitengo cha maendeleo ya jamii kuhakikisha wanawake wanajiunga kwenye jukwaa hilo kwani wakiwe kule wataweza kujifunza vitu vingi hata huu ukatili unaoendelea hatokuwepo.” Aliongeza.

Aidha, alisema ukatili kwa watoto na wanawake umeongezeka na kufanya wanawake wengi kudumaa kiuchumi huku takwimu zikionyesha kwa mwaka 2021 zaidi ya watoto 11490 sawa na asilimia 15 wamefanyiwa ukatilii.

Pia alisema serikali inakuja na mpango wa malezi ya mtoto ambapo itaanza kulea kuanzia miaka 3 hadi miaka 8 na baadae kuendelea na vijana kwa lengo la kuwavusha watoto na vijana kwenye janga la ubakaji na ulawiti ambao wamekuwa wakifanyiwa.

Akizungumza Kwa niaba ya Mkurugenzi wa chama Cha wanasheria wanawake TAULA,alisema Mila na desturi kandamizi kwa wanawake, miundombinu isiyo rafiki hasa kipindi Cha mvua, ukatili wa kijinsia pamoja na ndoa za utotoni zinachangia kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake waishio kijijini.

AIDHA alisema TAULA itaendelea kushirikiana na Serikali kupitia Halmashauri kutoa elimu ya msaada wa kisheria Kwa Wanwake hasa waishio Kijijini ili kuweka afua ya Changamoto wanazopitia na kuwainua kiuchumi.

Kaimu katibu Mkuu Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum, Sebastian Kitiku alisema Mkakati wa Wizara ni Kuwezesha wanawake kiuchumi, kutokomeza vitendo vya ukatili Kwa wanawake, kuongeza kazi ya uamuzi kwenye uongozi.

Akizungumza Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Fatma Mwassa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bi. Hanje Godigodi alisema kupitia maadhimisho hayo yatasaidia kuwakomboa wanawake wa kijijini kuweza kujinasua kwenye changamoto za unyanyasaji wa kijinsia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here