Home LOCAL WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUDHIBITI MOTO KWENYE MASHAMBA YA MITI

WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUDHIBITI MOTO KWENYE MASHAMBA YA MITI


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Mary Masanja(Mb) amewataka wananchi Mkoani Iringa kushirikiana katika kudhibiti matukio ya moto yanayojitokeza kwenye mashamba ya miti binafsi na ya Serikali.

Ameyasema hayo leo katika Kijiji cha Kibengu Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta katika Shamba la Miti Saohill.

“Niwaombe sana kila mtu awe mlinzi wa mwenzake, kama unaandaa shamba hakikisha unaangalia upepo unaelekea wapi ndipo uchome” amesisitiza.

Amewaomba wananchi kuwasiliana na viongozi wa mashamba inapofikia wakati wa kuandaa mashamba yao ili waweze kuwa karibu kudhibiti moto ambao unaweza ukajitokeza .

Amefafanua kuwa mashamba ya miti yamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi kwa kutoa ajira akitolea mfano wa Shamba la Miti Sao Hill ambalo limekuwa likitoa ajira zaidi ya 4000 kwa wananchi.

Amesema Shamba hilo pia limekuwa likisaidia katika huduma mbalimbali kwa jamii kama kusaidia ujenzi wa madarasa,zahanati, vituo vya afya pamoja na ujenzi wa shule

Aidha, shamba hilo pia
huzalisha Miche ya miti ipatayo milioni 7 kila mwaka ambayo hupandwa kwenye maeneo yaliyovunwa , huwagawia wananchi na Taasisi mbalimbali binafsi.

Ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta inaendelea mkoani Njombe Oktoba 25, 2022

Previous articleDAWASA YATOA RATIBA YA MGAO WA MAJI
Next articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 27-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here