Home LOCAL WAHENGA ALMINIUM WACHANGIA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU CCM MKOA

WAHENGA ALMINIUM WACHANGIA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU CCM MKOA

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar Es Salaam Mama Kate Kamba akisalimiana na Mkurugenzi wa kampuni ya Wahenga Aluminum John Ryoba Wilayani Kigamboni leo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo (Picha na Heri Shaaban )

Mkurugenzi wa Kampuni ya Wahenga John Ryoba akizungumza katika ziara ya Katibu MKuu wa CCM Daniel Chongolo Wilayani Kigamboni

Katibu wa chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Daniel Chongolo(katikati) akikata utepe wakati wa kuweka jiwe la Msingi Ofisi ya CCM WIlaya Kigamboni pamoja na nyumba ya Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam leo Octoba 21/2022 (kushoto)Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba (Picha na Heri Shaaban

Na Heri Shaaban (Kigamboni)

KAMPUNI ya Wahenga Aluminum iliyopo Kinyerezi imechangia asilimia 50 ya ujenzi wa Jengo la nyumba ya Katibu wa chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Dar es Salaam iliyopo Wilayaji Kigamboni .

Akitoa ahadi ya kuchangia gharama za Ujenzi Wilayani Kigamboni Mkurugenzi Kampuni ya Wahenga Aluminum John Ryoba , mbele ya mgeni rasmi Katibu Mkuu CCM Taifa Daniel Chongolo, wakati wa kuweka jiwe la Msingi la Ofisi ya CCM WIlaya Kigamboni na Nyumba ya Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.

“Leo ni siku ya kwanza kukutana na viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM nyumba za Dar es Salaam zote zimewekwa Aluminum na KAMPUNI yetu ya Wahenga ,Wahenga Aluminum tumesaidia Kata ,Wilaya na Mkoa kutatua changamoto mbalimbali kwa ajili ya kujenga chama Cha Mapinduzi CCM ,Kampuni yetu itasaidia kuchangia gharama za Ujenzi wa milango ya Aluminum na madirisha tutachangia asilimia 50 ya ujenzi sawa na shilingi milioni 4.8 “alisema John Ryoba

Mkurugenzi wa Wahenga John Ryoba alisema atashirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM kwa ajili ya kujenga Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumsaidia RAIS Samia Suluhu Hassan ,katika utekelezaji wa Ilani ya Chama .

Ryoba alisema yeye ni kada wa chama Cha Mapinduzi CCM anashirikiana na chama na Serikali katika kuleta maendeleo .

Naibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Ojambi Masaburi alisema atachangia shilingi milioni 5 gharama za Ujenzi huo pia atakuwa Mshauri Mkuu katika maswala ya Ununuzi wa vifaa vya ujenzi huo .

Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilayani Ilala kutoka Jumuiya ya Wazazi George Mtambalike alisema ataleta miti Kwa ajili ya utunzaji MAZINGIRA ya nyumba ya Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam .

Aliyekuwa Waziri wa Utumishi Hawa Ghasia alisema atachangia vifaa vyote vya umeme vya jengo hilo mpaka LIKAMILIKE .

Mwisho

Previous articleTPA KUANZISHA UTALII WA MELI NCHINI, YASHINDA TUZO ONESHO LA UTALII LA KIMATAIFA (S!TE) JIJINI DAR
Next articleSIMBA,YANGA WATUNISHIANA MISULI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here