Home LOCAL VIONGOZI MBALIMBALI WA CHAMA NA SERIKALI WAHUDHURIA MAZISHI YA DKT. MWINYIHAJI MAKAME...

VIONGOZI MBALIMBALI WA CHAMA NA SERIKALI WAHUDHURIA MAZISHI YA DKT. MWINYIHAJI MAKAME MWADINI ZANZIBAR

Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali wamehudhuria katika Mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe Nchini Mheshimiwa Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini Kijijini kwao Bweleo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Viongozi mbali mbali wamehudhuria katika katika mazishi hayo wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla.

Viongozi wengine waliohudhuria katika Mazishi hayo ni Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Sita Alhajj Dkt. Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Saba Alhajj Dkt. Ali Muhamed Shein, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Alhajj Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Alhajj Khamis Ramadhan Abdallah.

Wengine ni Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Mhe. Hafidh Ameir, Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Viongozi Vyama, Dini na Serikali, Wanafamilia, na Wananchi mbali mbali wa Zanzibar.

Akisoma Wasfu wa Marehemu Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini Katibu wa Tume ya Utumishi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndugu Mahmoud Ahmada Haji ameeleza kuwa Marehemu katika uhai wake amepata elimu ndani na nje ya nchi ameshika nafasi mbali mbali za Uongozi ikiwemo Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa vipindi Tofauti kupitia Chama Cha Mapinduzi, na aliwahi kuongoza Kamati mbali mbali za Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Aidha Marehemu amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Biashara (ZSTV).

Hadi kufariki kwake Marehemu alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Dkt. Mwinyihaji amefariki Dunia Usiku wa kuamkia leo baada ya Kuugua kwa Muda Mfupi na kuzikwa leo Kijijini kwao Bweleo.

Marehemu ameacha Kizuka Mmoja na watoto watano.

Innaa Lillaahi wainnaa Ilaihi Raajiun.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (AMPR)
21 Oktoba 2022

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here