Home BUSINESS TPA KUANZISHA UTALII WA MELI NCHINI, YASHINDA TUZO ONESHO LA UTALII LA...

TPA KUANZISHA UTALII WA MELI NCHINI, YASHINDA TUZO ONESHO LA UTALII LA KIMATAIFA (S!TE) JIJINI DAR

Mkuu wa Chuo cha Bandari Dkt. Hussein Lufunyo (kushoto) akiwa na Baadhi ya watumishi wa Chuo hicho katika picha picha ya pamoja mara baada ya kupokea Tuzo ya Mshindi wa Kwanza katika Onesho la S!TE Oktoba 22, katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. (wa kwanza kulia) ni, Afisa mafunzo wa Chuo cha Bandari Upendo Mtinangi. Mkuu wa Chuo cha Bandari Dkt. Hussein Lufunyo (mwenye suti nyeusi) akizungumzaa na baadhi ya watumishi wa wa Chuo hicho akiwapongeza mara baada ya kupata TUZO ya Mshindi wa kwanza katika Onesho hilo.

Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeibuka mshindi wa kwanza na kupata Tuzo katika Onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili (S!TE) linalofanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 21 hadi 23, 2022 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Onesho hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)  Plasduce Mbosa, Mkuu wa Chuo cha Bandari Dkt. Hussein Lufunyo amesema kuwa TPA imeshiriki katika Onesho hilo ikiwa ndio Mdhamini Mkuu na kwamba waliona upo umuhimu wa kushiriki kwakuwa  kuna uhusiano mkubwa kati ya Mamlaka hiyo na Sekta ya Utalii kwa ujumla.

“Kama mnavyofahamu Bandari ndio lango Kuu la uchumi wa nchi yetu na hivyo shughuli za Bandari zikiimarika  basi  hata uchumi katika shughukli za kitalii zitaimarika pia”amesema Dkt. Lufunyo.

Ameelezea kuwa Mamlaka hiyo licha ya kuwa na shughuli nyingi katika Bandari zake lakini kubwa ni kujihusisha na upakiaji pamoja na upakuaji mizigo na kwamba katika kutekeleza hilo ipo mizigo inayokwenda kutumika katika miundominu kwenye sekta ya utalii

Aidha ameelezea uwepo wa mradi mkubwa wanaoutekeleza  wa utalii wa meli ambao kwa sasa wanaboresha miundombinu ya Bandari itakayowezesha kupokea meli kubwa za kitalii ambapo watalii watapaki meli yao Bandalini wakati wakielekea kwenye maeneo mbalimbali ya kitalii na kisha wanarudi kuendelea na safari zao hivyo watakuwa wamejihakikishia usalama wa meli yao.

“Mradi huu ukikamilika tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye sekta nzima ya utalii. Tunaboresha miundombinu ya Bandari hasa geti la abiria la kuelekea Zanzibar ambapo tukiwa na miundombinu ya utalii wa meli watakapofika kwenye bandari yetu basi watalii hao watashuka kuelekeza Zanzibar na maeneo mengine ya utalii, na zile Meli zitaendelea kupaki Bandarini kuwasubiri huku wakiwa na uhakika mkubwa wa usalama wa meli zao” ameeleza Dkt. Lufunyo.

Ameongeza kuwa TPA wameshiriki kwenye tukio hilo kueleza wanachofanya katika kuunga mkono Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Kwakuzingatia kuwa hivi karibuni kulizinduliwa filamu ya ‘The Royal Tour’ na kwamba TPA imekuwa mdau mkubwa kwenye suala zima la utalii hapa nchini.

“kwa kuzingatia hilo mamlaka ya Bandari tuko hapa kuelezea muunganiko uliopo kati yetu na Bodi ya Utalii pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii na kutoa fursa kwa wananchi kufahamu mchango wetu katika sekta ya utalii kwa ujumla”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here