Home LOCAL TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI UTOAJI CHANJO YA UVIKO-19 AFRIKA 

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI UTOAJI CHANJO YA UVIKO-19 AFRIKA 

Na.WAF, Dodoma

Mratibu Kiongozi Kimataifa wa Ubia wa Utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 Bw. Ted Chaiban ameipongeza Tanzania na nchini nyingine Barani Afrika pamoja na wadau wa Sekta ya afya kwa uhamasishaji na kuchanja wananchi chanjo dhidi ya UVIKO-19.
 
Bw. Ted Chaiban amebainisha kuwa Tanzaina imeshika nafasi ya 2 kwa kiwango cha juu cha uchanjaji huku ikiwa imefikia asilimia 37.9 ya uchanjaji wananchi kwa mujibu wa takwimu za kidunia.

Katika kusisitiza hilo, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Wadau wa maendeleo, Watumishi wa afya na watu wengine waliowezesha kufanikisha jitihada hizi za kuwakinga wananchi dhidi ya UVIKO-19 na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya 2 Afrika kwa kiwango cha juu cha uchanjaji.

#UjanjaKuchanja #KingaNiBorakulikoTiba #MtuniAfya #JaliAfyaYako

Previous articleDKT. KIJAJI AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA STAKABADHI ZA GHALA (WRRB) JIJINI DAR
Next articleTUKAANZISHE KLINIKI ZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA- DKT. KENGIA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here