Home BUSINESS STAMICO YAWAPONGEZA WACHIMBAJI WADOGO KWA KUONGEZA KWA JITIHADA ZAO ZA KUKUZA SEKTA...

STAMICO YAWAPONGEZA WACHIMBAJI WADOGO KWA KUONGEZA KWA JITIHADA ZAO ZA KUKUZA SEKTA YA MADINI

Na: Hughes Dugilo, Geita.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Vennance Mwasse amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kutambua mchango wa wachimbaji wadogo na wadau wote waliopo katika sekta ya hiyo kwa kuendelea kuunga mkono kazi zao ili waweze kufikia malengo yao.

Dkt. Mwasse ameyasema hayo leo Octoba 2,2022 katika mahojiano maalum na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake fupi ya kutembelea mambanda mbalimbali katika Maoesho ya tano ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita

Katika Ziara hiyo, Dkt. Mwasse alipata fursa ya kuwatembelea wadau hao na kuwashukuru kwa kushiriki kikamilifu katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 yaliyofanyika mwezi Agosti Mwaka huu, mkoani Dodoma.

“Mwaka huu Shirika limefikisha miaka 50. huu ni umri mkubwa kufika hapa sio jambo rahisi. Hivyo tunatambua mchango wa wadau wengine katika sekta ya madini ndio maana katika maonesho haya tumetumia fursa hii kuwatembelea na kuwapa zawadi ya kumbukumbu ya maadhimisho hayo ili kuthamini mchango wao kwa Shirika letu” amesema Dkt. Mwasse

Amewata wataka wadau wote wa madini hususani wachimbaji wadogo kuendelea kushirikiana na STAMICO  wakati wote na kwamba Shirika lipo tayari wakati wote kutoa msaada wa kitaalamu na kutatua changamoto za kiuchimbaji pale zinapotokea.

katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amepokea Tuzo kutoka kwa Chama cha Wasanii Mkoani Geita (TDFAA) kwa kutambua mchango wa Shirika hilo katika maeneo mbalimbali ikiwemo kudhamini Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza alipokuwa akikabidhi Tuzo hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji wa Filamu Mkoa wa Geita (TDFAA) Rosemary Paul amesema kuwa wametoa Tuzo hiyo kutambua mchango wa Shirika hilo kwa namna linavyowaunga mkono katika kazi zao.

“Tumekabidhi Tuzo hii kwa Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse kwa mchango wake mkubwa wa kutambua na kuthamini shughuli tunazozifanya za sanaa hapa Mkoani kwetu”

“Lakini ombi letu kubwa tunamuomba Mkurugenzi asituache aendelee kutushika mkono na sisi kwa umoja wetu tunaendelea kuutangaza Mkaa Mbadala unaozalishwa na STAMICO ili wananchi wa Geita na Watanzania wote kwa ujumla wautumie”amesema Rosemary.

Previous articleWACHIMBAJI WADOGO WATAKIWA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA
Next articleZIARA YA MKUU WA MKOA WA GEITA KATIKA BANDA LA TUME YA MADINI NA TGC KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here