Home BUSINESS STAMICO YAONESHA MTAMBO WAKE WA KISASA UNAOFANYA KAZI YA UCHORONGAJI NA UTAFITI...

STAMICO YAONESHA MTAMBO WAKE WA KISASA UNAOFANYA KAZI YA UCHORONGAJI NA UTAFITI WA MADINI

Mtambo wa kisasa wa uchorongaji na utafiti wa madini aina Reverse Circulation ( RC).

NA: JOHN BUKUKU-GEITA

Msimamizi wa Mradi wa Uchongaji GGM kutoka Shirika la Taifa la Madini STAMICO Mark Andrew Magesa akionesha namna mtambo wa kisasa wa uchorongaji na utafiti wa madini  aina ya Reverse Circulation ( RC) unavyofanya kazi katika maonesho ya  Tano ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.

Msimamizi wa Mradi wa Uchongaji GGM kutoka Shirika la Taifa la Madini STAMICO Mark Andrew Magesa akiwa na mwenzake Sebastian Hoja kando ya mtambo huo.

Msimamizi wa Mradi wa Uchongaji GGM kutoka Shirika la Taifa la Madini STAMICO Mark Andrew Magesa akiwa na wenzake Sebastian Hoja kulia na Mark stephano  kutoka STAMICO kando ya mtambo huo.,

Huu ni mtambo unaoitwa Booster ambao unasaidia mashine ya uchorongaji kufanya kazi kwa nguvu zaidi katika mazingira miamba migumu.

GEITA.

Shirika la Taifa la Madini STAMICO limejipanga kuongeza mashine zaidi bora na za kisasa za uchimbaji Ili kuzidi kuimarisha huduma ya uchimbaji kwa wachimbaji wadogo.

Msimamizi wa Mradi wa Uchorongaji (GGM) kutoka Shirika la Taifa la Madini STAMICO Mark Andrew Magesa  ameeleza hayo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari katika Maonesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.

Amesema katika mradi wao wanafanya shughuli za Uchongaji kwa kutumia mashine tatu ambazo Mbili ni za Diamond Drill Rig na moja ya Reverse Circulation ( RC)  ambayo nayo inafanyakazi ya Uchorongaji.

Hii (RC) ni kwa ajili ya uchorongaji wa miamba mbali mbali Kwa ajili ya utafiti WA Madini ( Mineral Exploration) pamoja na uchimbaji wa ndani ya Pit ( Ore Development) RC inatoa (Sample) aina ya unga unga kama Chips mtambo huu  una uwezo wa kwenda mita zaidi ya 200

Lakini pia Kuna mitambo mingeni inaitwa Diamond Drilling Rig, ambayo (Sample) yake inatoka aina Core , mtambo una uwezo wa kuchoronga na kwenda zaidi mita 1000.

Amesema mtambo huo ni wa kisasa kutokana na kuendeshwa na rimoti tofauti na mitambo mingine ambapo Panel zake zipo kwenye mashine hivyo inasaidia kupunguza vihatarishi kwani mfanyakazi ana uwezo wa kukaa umbali mrefu kama mita kumi na zaidi akifanya kazi vizuri.

Magesa amesema mtambo huo unauwezo wa kufanya kazi zaidi ya mbili ikiwemo ya utafiti kwenye eneo ambalo hujawahi kulifanyia kazi ya uchimbaji madini kabisa lakini pia kuchimba sehemu yenye dhahabu Ili kuona muendelezo wa upatikanaji wa madini hayo katika eneo hilo.

Aidha ameeleza kuwa mtambo huo pia unaweza kufanya kazi sehemu yeyote bila kujali changamoto hasa ya maji kwa kiasi gani.

“Mpaka Sasa tunafanya kazi na migodi mitatu ukiwemo Mgodi wa Anglo Gold Ashanti (GGM),Mgodi wa Backreef Pamoja na Mgodi wa uchimbaji wa dhahabu wa Buhemba Gold Mine yote tunafanya kazi kwa ufanisi wa Hali ya juu”amesema Magesa

Magesa ameendelea kusema kuwa Shirika Hilo limeendelea kuongeza zaidi mashine 15 hivyo wanazitafutia Kazi li ziweze kuingia katika uperesheni na hivyo wanatarajia kuongeza mitambo mingine ya kisasa ili kuzidi kuimarisha huduma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here