Home Uncategorized SIMBA YAIPIGA MTIBWA 5-O

SIMBA YAIPIGA MTIBWA 5-O

Na: Mwandishi Wetu

KIKOSI cha Simba SC leo wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo, Mzawa Muzamil Yassin dakika ya 38, Msenegal Pape Ousmane Sakho mawili dakika ya 48 na 90 na ushei na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri mawili pia, dakika ya 63 na 73.

Kwa ushindi huo, Simba SC wanafikisha pointi 17 na kupanda nafasi ya pili, sasa wakizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi nane, wakati Mtibwa Sugar inayobaki na pointi zake 15 za mechi 10 wanashukia nafasi ya nne.

Mtibwa Sugar zilianza mapema tu dakika ya 37 baada ya kipa wake wa kwanza, Farouk Shikaro kuumia na kushindwa na kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Hamadi Kadedi.

Hali ikawa mbaya zaidi baada ya walinzi wake wawili wa kati kutolewa kwa kadi nyekundu wote mmoja kila kipindi, Mkongo Paschal Kitenge dakika ya 41 na Cassin Ponera dakika ya 67.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here