Home SPORTS SIMBA,YANGA WATUNISHIANA MISULI

SIMBA,YANGA WATUNISHIANA MISULI

Na Mwandishi Wetu

MTANANGE wa watani wa jadi Yanga na Simba umemalizika kwa sare ya 1-1, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba ilipata bao katika dakika ya 15 Augustine Okra akipokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama na kukwamisha mpira wavuni.

Katika mtanange huo ambao kwa zote kusomana huku kila mmoja akianza soka la taratibu huku kila mmoja akilinda goli lake na kushambuliana kwa kushituliza.

Katika dakika ya 45 mchezaji Stephan Aziz KI alipiga shuti kali nje ya 18 liliwatosha Yanga kwenda mapumziko kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba wakitumia dakika 30 kusawazisha.

Hata hivyo katika dakika tisini kwenye mchezo huo zimemfanya mwamuzi Ramadhan Kayoko kutoa kadi tisa za njano huku Yanga wakiongoza kwa kuonyeshwa kadi tano na Simba nne.

Kipindi cha pili Yanga waliuanza mchezo kwa kaso dakika 10 zakipindi cha pili baada ya hapo timu zote zilinza kucheza mpira wa kuviziana.

Dakika ya 47 Yanga ilipata kona lakini haikuwa na faida kwao kutokana na kuokolewa na mabeki wa Simba wakiongozw na Joash Onyango ambaye alimnyima zaidi nafasi ya kutetema Fiston Mayele.

Kipindi cha pili kona nne zilichongwa Simba wakipata tatu na zote hazikuwa na madhara langoni mwa waponzani na Yanga walipata moja.

Timu zote zilifanya mabadiliko kwa upande wa Yanga walitoka Jeses Moloko, Kisinda nafasi zao zilichukuliwa na Farid Mussa, Gael Bigirimana na

Kwa upande wa Simba alitoka Sakho, Okra na Mwenda nafasi zao zilichukuliwa na Nyoni, Kyombo na Kibu.

Katika mchezo huo Simba inabaki kileleni na Yanga ikiwa nafasi ya pili na timu zote zimefikisha jumla ya alam

Previous articleWAHENGA ALMINIUM WACHANGIA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU CCM MKOA
Next articleRAIS SAMIA PAMOJA NA MGENI WAKE RAIS WA DR CONGO FÉLIX TSHILOMBO WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here