Home SPORTS SIMBA SC YAFUZU HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA SC YAFUZU HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

KLABU ya wekundu wa msimbazi Simba SC imefanikiwa kufuzu  hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu  ya  de Agosto ya nchini Angola.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam timu ya Simba ilipata bao la kuongoza na la ushindi katika dakika chache kabla ya mchezo huo kwenda mapumziko goli lililofungwa na mshambuliaji machachari raia wa Zambia Mosses Phil.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote mbili kushambuliana lango la mwenzake lakini mpaka refa anapuliza kipyenga cha mwisho timu ya de Agosto hawakufanikiwa kupata goli.

Kufuatia mchezo huo timu ya Simba SC imefuzu kwenda hatua ya makundi kwa jumla ya magoli  4-1 Kufuatia mchezo wa awali Simba kushinda magoli 3-1 ikiwa ugenini nchini Angola baada ya mechi ya kwanza Simba Sc kushinda 3-1 ugenini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here