MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hemed Suleiman Abudulla akipiga kura kuchagua viongozi wapya wa CCM awialaya ya Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi, wakati wa Uchaguzi uliofanyika leo Oktoba 2, 2022. (Picha na Fahad Siraji wa CCM).
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akipiga kura kuchagua viongozi wapya wa CCM Wilaya ya Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi, wakati wa Uchaguzi uliofanyika leo Oktoba 2, 2022. (Picha na Fahad Siraji wa CCM).
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi, wakiwa katika matukio tofauti wakati wa uchaguzi wa viongozi wapya wa CCM katika Wilaya hiyo uliofanyika leo Oktoba 2, 2022. (Picha na Fahad Siraji wa CCM).
**********
*Asema upo umuhimu wa viongozi wapya kujengewa uwezo ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
Â
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema Chama kimeona umuhimu wa kuwajengea uwezo viongozi wote wapya ndani ya Chama na kwamba baada ya Kukamilika kwa Uchaguzi unaondelea watapatiwa mafunzo ili watekeleze majuku yao kwa ufanisi.
Â
Aidha, amesema CCM bado ni eneo muhimu katika kuzalisha viongozi bora na tegemeo kwa maendeleo ya nchi.
Â
Shaka ameyasema hayo aliposhiriki mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa CCM Wilaya ya Dimani, Mkoa wa Mjini Magharibi ambao umefanyika leo Oktoba 2, 2022.
Â
Asema viongozi wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia mipaka kulingana na Katiba ya CCM, kanuni na miongozo ya Chama, hivyo ili kwenda sawasawa ni lazima kuishi ktika misingi ya Katiba, kanuni na utaratibu.
Â
“Ndugu zangu wengi tuliopo hapa ni viongozi wapya, tumekabidhiwa dhamana hii muhimu ya uongozi, Chama kimeweka mpango maalumu, ndani ya muda mfupi kuwapatia semina viongo katika ngazi zote,” amesema Shaka.