Home BUSINESS RC SHIGELA ATEMBELEA BANDA LA BoT MAONESHO YA MADINI GEITA

RC SHIGELA ATEMBELEA BANDA LA BoT MAONESHO YA MADINI GEITA

Graciana: Afisa Uhusiano kwa Umma wa Benki kuu ya Tanzania, Bi. Beatrice Ollotu (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela (kushoto) katika Banda la Benki kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Prof. Godius Kahyarara.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela (wa kwanza kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Msaidizi, Upatikanaji na Usimamizi wa Akiba ya Fedha za Kigeni, Dr. Anna Lyimo, kuhusu jinsi ambavyo Benki kuu ya Tanzania imejipanga kuwa na akiba ya kutosha fedha kigeni.

Meneja Msaidizi, Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Issa Pagali (Kushoto) akitoa elimu kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Prof. Godius Kahyarara alipotembelea banda la Benki kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Uhusiano kwa Umma wa Benki kuu ya Tanzania, Bi. Beatrice Ollotu (kulia) wakati RC Shigela alipotembelea Banda la Benki kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika uwanja wa Bombambili, uliopo Geita mjini, Mkoani Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Reuben Shigela akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Madini, mara ya kuhitimisha kutembelea mabanda yote ya Washiriki katika maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita. Maonesho haya yaliyoanza yanzu Septemba 27, 2022 yanafunguliwa rasmi leo Oktoba 3, 2022 na yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 8, 2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here