Home LOCAL RAIS SAMIA PAMOJA NA MGENI WAKE RAIS WA DR CONGO FÉLIX TSHILOMBO...

RAIS SAMIA PAMOJA NA MGENI WAKE RAIS WA DR CONGO FÉLIX TSHILOMBO WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakati wakishuhudia uwekaji saini Mkataba wa makubaliano baina ya Tanzania na DRC, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022. Kwa upande wa Tanzania, Mkataba huo ulisainiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye na kwa upande wa DRC uliwekwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Christophe Lutundula. 

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilomboakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.

Previous articleSIMBA,YANGA WATUNISHIANA MISULI
Next articleWANAFUNZI WALIOSOMA RUVU SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA UZIO WA SHULE HIYO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here