– Ni Baada ya mwenge kukataa kuzindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye Miraidi 65 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 12 iliyogubikwa na dosari ikiwemo Rushwa, Uzembe na Ubadhirifu.
– Miradi 1,263 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 650 imepitiwa na Mwenge wa uhuru 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehitimisha Kilele Cha Mbio za Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2022 ambapo ameelekeza TAKUKURU na ZAECA kufanya Uchunguzi na kuchukuwa hatua stahiki kwa wote waliobainika kufanya ubadhirifu wa fedha za umma kwenye Miradi 65 iliyokataliwa na Mwenge Baada ya kubainika kuwa na dosari ikiwemo Rushwa Uzembe na Ubadhirifu.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo wakati wa hitimisho la kilele Cha Mwenge wa uhuru 2022 iliyokwenda sambamba na kumbukizi ya miaka 23 ya kifo Cha hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Uwanja wa Kaitaba Kagera.
Hatua hiyo imekuja Baada ya Rais Samia kupokea taarifa nzima ya Mbio za Mwenge ambapo miradi 65 kutoka Halmashauri 43 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 12 ilibainika kuwa na dosari ikiwemo Ujenzi Chini ya kiwango, Rushwa,uzembe na ubadhirifu na ukiukwaji wa mikataba.
Aidha Rais Samia ameelekeza kila Kiongozi kuhakikisha anasimamia Matumizi sahihi ya Fedha zinazotolewa kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuhakikisha inafanyika kwa kuzingatia ubora kulingana na thamani ya Fedha.
Pamoja na hayo Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania kuyaenzi Mema na Mazuri tuliyoachiwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo kuikataa Rushwa, Uzembe na Ubadhirifu wa fedha za umma.
Hata hivyo Rais Samia amewapongeza Viongozi wa Mbio za Mwenge kwa uaminifu na uzalendo mkubwa walioonyesha ikiwa ni pamoja na kuikataa miradi yenye Mashaka na dosari.
Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2022 umekimbizwa kwa siku 195 kwenye Halmashauri 195 na kuweka mawe ya Msingi na kuzindua Miradi 1,263 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 650 Chini ya wakimbiza mwenge 6.