Home LOCAL PROF. ABOUD: WIZARA YA AFYA IMEENDELEA KUCHUKUA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO...

PROF. ABOUD: WIZARA YA AFYA IMEENDELEA KUCHUKUA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO MIPAKANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Aboud akizumza katika hafla ya makabidhiano makabidhiano ya  vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi  milioni 180 kwa ajili ya kuimarisha huduma za Afya katika mipaka iliyofanyika katika Ofisi za NIMR Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mipango wa CDC Dkt. George Mgomelle ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo akizungumza katika hafla hiyo.

Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la MDH, Dkt. David Sando akizungumza katika hafla hiyo na kutoa shukurani zake kwa wizara ya afya kwa kuonesha ushirikiano mkubwa.

Watumishi kutoka Wizara ya Afya, MDH, CDC, pamoja na waandishi wa habari katika katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Aboud akipokea vifaa mbalimbali kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la MDH, Dkt. David Sando kwa ajili ya ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko katika mipaka nchini katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika NIMR jijini Dar es Salaam leo.

Katika kukabiliana na tishio la magonjwa ya mlipuko mipakani , viwanja vya ndege na bandari, Serikali kupitia wizara ya Afya imepokea Vifaa mbalimbali vitakavyowezesha kuimarisha huduma za afya sambamba na kufuatilia taarifa za wasafiri.

Akizungumza leo Oktoba 29,2022 Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu (Mb), wakati wa kupokea vifaa mbalimbali vitakavyotumika kuimarisha huduma za Afya katika mipaka, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Aboud amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya afya imeendelea kuchukua hatua za kuthibiti magonjwa ya mlipuko katika mipaka, bandari na viwanja vya ndege kwa kuhakikisha magonjwa hayo yanadhibitiwa.

Prof. Aboud ameeleza kuwa vifaa hivyo vya kielektoniki vyenye thamani ya zaidi ya milioni 180 vimetolewa na kituo cha kudhibiti na kuzuia magojwa (CDC) kwa kushirikiana na Shirika la MDH.

Wizara ya Afya imepokea vifaa mbalimbali vya kielektroniki, vyumba vya uchunguzi (Booth), na Thamani (meza na viti) kutoka katika kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) kupitia shirika lisilo la kiserikali la MDH kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya katika mipaka yetu , bandari na viwanja vya ndege nchini amesema Prof. Aboud.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la MDH, Dkt. David Sando amesema kuwa vifaa hivyo vitatumika pia katika utunzaji wa kumbukumbu na takwimu mbalimbali zitakazotumika na wizara kufanya ufuatiliaji wakati kutakapotokea majanga ya magonjwa ya mlipuko.

Previous articleWABUNGE WAPYA WA BUNGE LA AFRIKA ‘PAP’ WAPEWA SEMINA ELEKEZI
Next articleAGIZO LA RAIS SAMIA LA KUBORESHA LISHE SIO LA WAKUU WA MIKOA TU, BALI NI LETU VIONGOZI WOTE – DKT. MOLLEL
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here