Home BUSINESS NHC KUANZA KAMPENI YA KUDAI MADENI KWA WADAIWA SUGU

NHC KUANZA KAMPENI YA KUDAI MADENI KWA WADAIWA SUGU

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya akizungumza na waandishi wa habari (awamo pichani) kuhusu kuanza kwa kampeni ya ukusanyaji madeni kwa wateja wao. MKutano huo umefanyika leo Oktoba 30,2022 katika Ofisi za Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (awamo pichani) katika mkutano huo. (kushoto) ni, Meneja Makusanyo Madeni chechefu Levinico Mbilinyi, na (kulia) ni, kaimu Mkurugenzi wa usimamizi – miliki wa NHC Eliah Msese.

kaimu Mkurugenzi wa usimamizi – miliki wa NHC Eliah Msese alifafanua jambo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi katika mkutano huo.

Meneja Makusanyo Madeni chechefu  wa NHC Levinico Mbilinyi (kushoto) akielezea namna ambavyo Shirika litatekeleza zoezi hilo kwa mujibu wa sheria.

Waandishi wa habari

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

DAR ES SALAAM.

Shirika la Nyumba la Taifa NHC limetangaza kuanza kampeni ya kudai madeni ya Kodi kwa wadaiwa sugu kwa wapangaji waliopo na waliohama kwenye nyumba za Shirika hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo Oktoba 30,2022 kwenye Ofisi za Shirika hilo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Shirika hilo Muungano Saguya amesema kuwa Shirika linawafahamisha wananchi wote kuanza kwa  kampeni mpya yenye lengo la ukusanyaji wa madeni hayo.

Aidha Saguya amefafanua kuwa Shirika linatoa muda wa siku sitini (60), kuanzia tarehe 01/11/2022 mpaka 30/12/2022  kwa wapangaji waliopo kwenye nyumba (Active tenants) na wapangaji waliohama (Ex-tenants) wanaodaiwa malimbikizo ya kodi hadi sasa uhakikisha  wamelipa malimbikizo yote wanayodaiwa ili kuepuka kuchukuliwa hatua stahiki.

Aidha Shirika linashirikiana na vyombo vingine vya dola kuhakikisha kuwa wapangaji hao wanapatikana na wanalipa kodi zao.

Amesema kuwa  kwa wapangaji ambao walishapewa notisi mbalimbali  utekelezaji utaendelea kama notisi hizo zinavyoelekeza. Hivyo Shirika linawasihi watekeleze wajibu wao kuepuka kadhia zitakazoweza kujitokeza kwa kushindwa kufanya hivyo.

“Kwa waliokuwa wapangaji ambao wamehama na kuacha madeni (Ex-tenants) wanayodaiwa, wanatakiwa kufika katika Ofisi za Shirika zilizo karibu nao na kupewa utaratibu wa malipo ikiwemo (control number) ili waanze kulipa” amesema Saguya, na kusisitiza kuwa,

“kwa wale watakaoshindwa kutekeleza ndani ya muda uliotolewa, Shirika litawatangaza kwenye vyombo vya habari ili watanzania wawafahamu watu wanaokwamisha Shirika  na watachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani.

“Kitendo cha wapangaji hao kukimbia na madeni ya nyumba ni sawa na uhujumu ambao hautavumiliwa na kwamba Shirika linaenda kuwasaka popote walipo kwa kutumia mbinu mbalimbali” amesisitiza.

Aidha amesema Shirika limekuwa likidai madeni ya kodi kwa kutumia mbinu mbalimbali ambapo  juhudi hizo zimesaidia kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 5 huku kiasi cha shilingi bilioni 21 zikiwa bado hazijakuswanywa.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa usimamizi – miliki wa NHC, Eliah Msese amewaasa watanzania wote kutotumia vishoka wanaojifanya kutoa msaada wa upatikanaji wa nyumba za Shirika hilo, na badala yake kufikia katika Ofisi za Shirika hilo zilizopo nchi nzima Ili kuwa na uhakika wa umuliki wa nyumba hizo.

Amesema kuwa upo utaratibu mzuri uliowekwa wa kuhakikisha mwananchi anapata nyumba bila kutumia vishoka na kwamba kwa Kufuata utarabu huo kutasaidia Kuondokana na tatizo la vishoka.

Kampeni hiyo ya miezi miwili itaongozwa na Kauli mbiu ya “LIPA KODI YA NYUMBA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU’’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here