Home LOCAL MWANAFUNZI KIDATO CHA 3 AFARIKI KWA KUNYWA SUMU YA PANYA GEITA.

MWANAFUNZI KIDATO CHA 3 AFARIKI KWA KUNYWA SUMU YA PANYA GEITA.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Nyabubele iliyopo wilayani Geita Mkoani Geita alietambulika kwa jina la Janeth Charles mwenye umri wa miaka 18 amefariki dunia baada ya kudaiwa kunywa sumu ya panya.

Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Nyakahongola Kata ya Kasamwa wilayani Geita mkoani Geita ambapo mwanafunzi huyo amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Nyakahongola iliyopo kata ya Kasamwa wilayani Geita.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Nyakahongola Poul Mgini amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi huyo huku akisema baada ya kumpokea mgonjwa huyo walimfanyia vipimo lakini wakati wakimhoji aliwaambia kuwa alikunywa sumu ya panya hali iliyopelekea kifo cha mwanafunzi huyo.

Akizungumza na Swahilitimes Baba mzazi wa binti huyo Charles Lugwesa amesema mwanao alianza hutapika na kuhalisha akiwa nyumbani ndipo walipomchukua na kumpeleka katika zahanati ya Nyakahongola kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Amesema wakati binti yao akiendelea kupatiwa matibabu katika zahanati ya Nyakahongola ndipo aliwaambia waauguzi kuwa alikunywa sumu ya panya huku wakiwa hawatambu sababu za binti yao kunywa sumu hiyo.

Juhudi za kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita bado zinaendelea.

Previous articleRAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA – MAJALIWA
Next articleWAZIRI GWAJIMA AWAONYA WANAOWATUMIA WATOTO KUJIPATIA KIPATO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here