*Shigella atoa Ofa kwa wawekezaji kumi wa mwanzo*
Na: Mwandishi wetu, GEITA
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kununua mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe unaotekelezwa na Shirika hilo.
Mbibo amenunua mkaa huo baada ya kushiriki katika Siku ya Geita iliyotanguliwa na kongamano la uwekezaji na baadaye kutembelea banda la STAMICO katika Maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini.
Aidha, Mbibo ametoa wito kwa STAMICO kuendelea kuutangaza mkaa huo ili wananchi waweze kuutambua na kuutumia kwa lengo la kuepusha ukataji wa miti na uharibifu wa mazingira.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella amezindua Jarida maalumu linaloangazia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ndani ya mkoa wa Geita.
Sambamba na hayo, Shigella amewaomba wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo mkoani humo ambapo ametoa ofa kwa wawekezaji kumi wa mwanzo watapatiwa eneo la kuwekeza bila malipo.
Maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yanatarajiwa kufungwa Oktoba 08, 2022.