Home LOCAL MAKAMU WA RAIS ATOA SALAMU ZA SERIKALI IBADA YA KUMUOMBEA BABA WA...

MAKAMU WA RAIS ATOA SALAMU ZA SERIKALI IBADA YA KUMUOMBEA BABA WA TAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Mpango akitoa salamu za serikali kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa Ibada maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Mjini Bukoba Mkoani Kagera leo tarehe 14 Oktoba 2022.

BUKOBA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa watanzania kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo ikiwemo kufanya kazi kwa bidii pamoja na kupinga vikali Rushwa.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akitoa salamu za serikali kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa Ibada maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Mjini Bukoba Mkoani Kagera leo tarehe 14 Oktoba 2022.

Amesema katika kumuezi Hayati  Baba wa Taifa ni lazima kuendelea kusisitiza amani na umoja kwa watanzania pamoja na bara la Afrika kwa ujumla.

Aidha ametoa wito kwa viongozi kuendelea kufanya kazi kwa kutenda haki, kugfanya kazi kwa uadilifu na kuondokana na Rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Makamu wa Rais amewaasa watanzania kufanya bidii katika masomo ili taifa liweze kupata wataalamu watakaotoa msaada katika mambo mbalimbali nchini.

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito kwa watanzania kutafuta hekima za Mwenyezi Mungu wakati wote wa kutekeleza majukumu kama alivyofanya Hayati Baba wa Taifa enzi za uhai wake.

Ibada maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere imeongozwa na Askofu wa Kanisa Kuu Katoliki Jimbo la Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango, Familia ya Baba wa Taifa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara Makongoro Nyerere, Mawaziri mbalimbali, Mkuu wa Mkoa Kagera , Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali, dini na vyama vya siasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here