Home BUSINESS KAMPUNI YA GEWOMA GOLDMINE LTD YAVUMBUA MADINI YA KAOLINE KANDA YA ZIWA

KAMPUNI YA GEWOMA GOLDMINE LTD YAVUMBUA MADINI YA KAOLINE KANDA YA ZIWA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni wa Kampuni ya Gewoma Goldmine Company Limited Bi. Josepha Woiso (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wengine wa Kampuni hiyo wakiwa katika Banda lao katika Maonesho ya Teknolojia katika Sekta ya Madini Mkoani Geita. (wa kwanza kulia) ni, Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Hellen Maduhu. wengine ni wajumbe wa Bodi wa Kampuni hiyo. (Kutoka kushoto), ni Johnson Manyanga. (anayefuata) ni, Honoratha Shirima, Kang’wa Mushosha, na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Geremia ndaki.

GEITA.

Gewoma Goldmine Company Limited ni kampuni ya wachimba madini mkoani Geita ambayo hivi Sasa imewekeza kwenye uchimbaji wa madini ya viwanda aina ya kaolin.

Madini ya kaoline yanatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani ikiwemo saruji, vyombo vya udongo, vigae, rangi za nyumba, dawa, mbolea dawa za mswaki.

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo Hellen Maduhu mesema anayofuraha kushiriki katika maonyesho ya tano ya trknolojia ya madini na kua Kampuni pekee iliyoweza kuonyesha madini aina ya kaolini yanayotumika katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani.

Kutokana na uwepo wa utajiri mwingi wa madini aina ya kaolini Kanda ya ziwa ambayo kampuni hiyo imeyabaini, Kampuni Sasa inakaribisha wawekezaji mbali mbali wa viwanda vya saruji, vigae na malighafi nyinginezo ili kuwekeza

Previous articleWAZIRI WA MADINI ARIDHISHWA KAZI YA UJENZI WA KITU CHA KUPOZA UMEME
Next articleRAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA FEDHA WA QATAR AMBAYE PIA NI MWENYEKITI  WA KATARA HOSPITALITY MHE. ALI BIN AHMED AL KUWAR, DOHA NCHINI QATAR 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here