Home BUSINESS HEKTA 372,000 ZA MISTU HUPOTEA KILA MWAKA NCHINI

HEKTA 372,000 ZA MISTU HUPOTEA KILA MWAKA NCHINI

Dkt. Masota Abel Kamishina Msaidizi TFS

Prof. Godius Kahyarara Katibu tawala Mkoa wa Geita

Asia Masima Mwenyekiti wa GEWOMA

Kamishina Msaidizi wa TFS Dkt. Masota Abel akipanda mti katika zoezi la upandaji miti lilifanyika Kwenye viwanja vya EPZA Bombambili Mkoani Geita.

Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Prof. Godius Kahyarara akipanda mti katika zoezi la upandaji miti lilifanyika Kwenye viwanja vya EPZA Bombambili Mkoani Geita.

Na: Costantine James, Geita.

Kamishina msaidizi wa Wakala wa huduma za Misitu Tanzani (TFS) Nchini Dkt. Masota Abel amesema zaidi ya hekta 372,000 zinapotea kila mwaka kutokana na uhalibifu wa misitu unaofanya na shughuli mbalimbali za kibinadamu.

Amesema hayo wakati aliposhiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la EPZA Bombambili mkoani Geita amesema sekta ya madini inachangia kwa kiasi kikubwa katika uhalibifu wa Misitu, Kilimo pamoja na ukataji miti kwa ajili ya matumizi ya kuni pamoja na uchomaji mkaa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Amesema kama taifa wanachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuongeza kasi ya upandaji miti kwenye maeneo ambayo yamehalibiwa pamoja na kusimamia sheria ili kulinda misitu ya asili iliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini isihalibiwe.

Katibu tawala wa Mkoa wa Geita prof. Godius Kahyarara amesema kutokana na shughuli za madini kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uhalibifu wa misitu hapa nchini amewataka TFS kuwekeza katika teknolojia ya vifaa vya utambuzi wa madini mahali yalipo ili kupunguza adha ya ukataji miti inayofanywa na wachimbaji wa madini katika utafutaji wa madini.

Prof. Kahyarara amesema Mkoa wa Geita umeamua kujikita zaidi katika matumizi ya teknolojia kwenye shughuli za uchimbaji wa madini katika mkoa huo kwa lengo kupunguza uhalibifu wa misitu uanotokana na shughuli za uchimbaji wa madini.

Amesema matumizi ya teknolojia katika uchimbaji wa madini kutasaidia pakubwa kupunguza uhalibifu wa misitu inayofanywa katika shughuli za uchimbaji wa madini.

Mwenyekiti wa wachimbaji wanawake Mkoa wa Geita Asia Masimba amekiri kuwa ni kweli wachimbaji wa madini wanachangia kwa kiasi kikubwa katika uhalibifu wa misitu ameishukuru TFS kutokana na kuwapa miti kwa lengo la kupanda katika sehemu wanazofanya shughuli zao ili kupunguza uhalibifu wa misitu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here