Home LOCAL DC MTATIRO ATAKA KASI YA UPANDAJI MITI TUNDURU KUWA AJENDA YA KUDUMU,AWAONGOZA...

DC MTATIRO ATAKA KASI YA UPANDAJI MITI TUNDURU KUWA AJENDA YA KUDUMU,AWAONGOZA WAUMINI NA VIONGOZI WA KANISA LA UPENDO WA KRISTO MASIHI KUPANDA MITI

Katibu wa Askofu wa Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Kiuma  wilani  Tunduru Fulko Hyera wa  kwanza kulia, na mwakilishi wa Shirika la Word & Deed la Ujerumani Susann Diechmanna wa pili kulia  wakimsikiliza  Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius  Mtatiro baada ya kumalizika  kwa zoezi la upandaji miti  katika viwanja vya  Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi  Kiuma wilayani humo, wa pili kushoto Mbunge wa Jimbo la Tunduru  Kaskazini Hassan Kungu.

Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Hassan Kungu akimwagilia maji kwenye mti baada ya kupanda wakati wa zoezi la uandaji miti lililofanyika katika viwanja vya Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Kiuma wilayani Tunduru.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro, akimwagilia maji mti alioupanda  wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti  lililofanywa na Taasisi ya Kiuma wilayani humo,kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Daniel Malukuta.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro kushoto na Katibu Mkuu wa  Taasisi ya Kiuma Daniel Malukuta wakipanda mti wa kivuli katika viwanja vya Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Kiuma wilayani Tunduru.

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kiuma Daniel Malukuta kulia, akimsaidia mwakilishi wa Shirika la Word& la Nchini Ujerumani Deed Susanna Diechmanna kupanda mti wa kumbukumbu  wakati wa zoezi la upandaji miti katika viwanja vya kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Kiuma.

Na: Muhidin Amri, Tunduru

MKUU wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro amesema,ni muhimu suala la upandaji miti katika wilaya hiyo liwe endelevu na jambo la mara kwa mara ili kusaidia uhifadhi wa mazingira.

Mtatiro amesema hayo,baada ya kuongoza zoezi la upandaji  miti lililofanyika katika eneo la Kanisa la Upendo la Kristo Masihi (KIUMA) kata ya Matemanga wilayani humo.

Mtatiro,amewakumbusha viongozi wa ngazi za vijiji,kata na Halmashauri  kuendelea kuhamasisha wananchi kupanda miti katika maeneo yao na kushauri aina ya miti inayofaa ambayo haina athari kimazingira hasa kwenye vyanzo vya maji.

Alisema,uharibifu wa mazingira unaongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na shughuli za kibinadanu ikiwamo kilimo na ufugaji holole, huku waharibifu hao wakishindwa kupanda miti mipya katika maeneo hayo,jambo linalo weza kuhatarisha maisha ya binadamu na viumbe hai wengine.

Alisema,suala la upandaji miti ni muhimu katika jamii yetu kwani itasaidia sana kukabiliana na changamoto ya hewa ukaa inayoweza kuhatarisha maisha ya Binadamu,hivyo wananchi wana wajibu wa kuzuia hatari  hiyo.

Aidha,amelipongeza kanisa hilo kwa kuandaa zoezi la upandaji miti na kuzitaka taasisi nyingine za dini,serikali na binafsi kuiga mfano wa Kanisa la Upendo kutokana na harakati zake  za kupanda miti mara kwa mara ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Alisema,serikali imekuwa na mikakati mbalimbali katika kuhakikisha inatunza mazingira ambapo alitaja miongoni mwa mikakati hiyo ni kupanda miti kwa wingi katika taasisi,idara za serikali na  taasisi binafsi.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini Hassan Kungu alisema,amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji mazingira kwa kupanda miti kwa wingi katika maeneo yao.

Naye Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kiuma Daniel Malukuta alisema,kila mwaka taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kuotesha miche na kupanda miti kuzunguka maeneo yake ili kutunza mazingira na kuhamasisha jamii na waumini wa kanisa la Upendo kuona suala la upandaji miti ni muhimu katika maisha yao.

MWISHOO

Previous articleKATA 4 KUNUFAIKA NA MRADI WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
Next articleWAZIRI MKUU ATEMBELEA ENEO YANAPOJENGWA MABEHEWA YA SGR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here