Na: HERI SHAABAN (Ilala)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija ametoa wiki tatu Soko la Kigogo Fresh liwe limekamilika lianze kutoa huduma .
Mkuu wa Wilaya Ludigija alitoa agizo hilo katika ziara yake endelevu ya kutatua kero na kukagua Miradi ya Maendeleo muendelezo ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.
“Nauagiza Uongozi wa Soko la Kigogo Fresh kuweka Utaratibu mzuri na kuwaruhusu Wafanyabiashara waanze kutumia Miundombinu mipya ya Soko hili mapema wiki hii ndani ya wiki tatu soko jingine liwe limekamilika “ alisema Ludigija .
Aidha Ludigija amewataka wana Ilala kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuendelea kuweka miundombinu mizuri na rafiki kwa wafanyabiashara haswa wadogowadogo.
Aliwataka Wananchi wa Wilaya ya Ilala kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda .
Mwisho