Home BUSINESS BRELA YAAGIZWA KUTOZIFUNGA KAMPUNI ZINAZODAIWA

BRELA YAAGIZWA KUTOZIFUNGA KAMPUNI ZINAZODAIWA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilipopokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya BRELA. Kilichofanyika Leo Oktoba 26,2022 Jijini Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa akizungumza wakati Akijibu baadhi ya maswali ya Wajumbe wa Kamati hiyo.

PICHA MBALIMBALI ZA WAJUMBE WA KAMATI

(PICHA ZOTE NA: BRELA)

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ametoa agizo kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kutozifunga kampuni zinazodaiwa badala yake kukaa na Wafanyabiashara na kutatua changamoto walizonazo katika masuala ya Leseni na Usajili wa Makampuni ili kuboresha Mazingira ya Biashara.

Mhe. Dkt. Kijaji ametoa agizo hilo tarehe 26 Oktoba, 2022 jijini Dodoma, wakati wa kikao cha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilipopokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya BRELA.

Mhe. Dkt. Kijaji Ameeleza kuwa Serikali imeendelea kutengeneza Mazingira ya Biashara kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara BLUEPRINT hivyo ameitaka BRELA kuendelea kutoa elimu ya Usajili wa Makampuni, Leseni na Umiliki Manufaa.

Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma za BRELA ikiwemo Uwasilishaji wa taarifa za wamiliki manufaa, uhusiano wa biashara kati ya Tanzania Bara na Zanzibar na Sheria ya Leseni za Biashara na usajili wa viwanda ya mwaka 1967 ambayo inauhitaji mkubwa wa kuifanyia marekebisho.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile (Mb) ameipongeza BRELA kwa kazi nzuri na kusema kuwa ni wakati sasa wa Wizara kuzileta pamoja taasisi zake za BRELA, EPZA na TIC ambazo zinahusika na utoaji wa Leseni au vibali ili kuwa na takwimu sahihi za Wafanyabiashara Nchini nzima.

Akijibu baadhi ya maswali ya Wajumbe wa Kamati hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa ameahidi kuwa BRELA itaendelea kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utoaji wa huduma na kutumia mifumo ya Kielektroniki ya Utoaji Huduma za Sajili (ORS) na Utoaji wa Leseni za Biashara (NBP).

Awali akiwasilisha taarifa ya usajili wa Makampuni pamoja na jukumu la utoaji Leseni Kaimu Mkuu wa sehemu ya Makampuni BRELA Bi. Leticia Zavu amesema kuwa BRELA imekuwa ikitoa elimu ya mara kwa mara kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwa waliosajili kampuni, kampeni juu ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA na ukaguzi elimishi kwa kuwatembelea Wafanyabiashara kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 26-2022
Next articleRAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA – MAJALIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here