Home BUSINESS BoT YATEMBELEWA NA UJUMBE KUTOKA SERIKALI YA ZAMBIA

BoT YATEMBELEWA NA UJUMBE KUTOKA SERIKALI YA ZAMBIA

Meneja Msaidizi, Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Issa Pagali (Kulia) akimweleza Mwakilishi wa Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zambia, Kennedy Mumba, mchango wa Benki kuu ya Tanzania katika ukuaji wa sekta ya Madini nchini wakati Mwakilishi huyo alipotembelea Banda la Benki kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Bombambili mkoani Geita.

Mwakilishi wa Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zambia, Bw. Kennedy Mumba (Kushoto), akiuliza swali kwa Meneja Msaidizi Uchumi nq Takwimu wa Benki kuu ya Tanzania alipotembelea Banda la BoT katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Bombambili mkoani Geita. Bw. Mumba alitaka kujua ni kwa vipi BoT inachangia katika ukuaji wa Sekta ya Madini nchini.

Maafisa wa Benki Kuu ya Tanzania (Kulia) wakifurahia jambo wakati wakitoa elimu kwa Wananchi wa Mkoa wa Geita waliofika katika Banda la Benki kuu ya Tanzania katika Maonesho ya tano ya Teknoloji ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Bombambili Mkoani Geita.

Meneja Msaidizi, Upatikanaji na Usimamizi wa Akiba ya Fedha za Kigeni, Dr. Anna Lyimo akitoa elimu kuhusu hati fungani kwa mkazi wa Geita aliyefika katika Banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanaayoendelea katika Uwanja wa Bombambili Geita.

Afisa wa Benki kuu ya Tanzania, Miriam Mgina (Kulia) akitoa elimu ya utambuzi wa alama za usalama katika fedha (noti) halali za kitanzania.

Afisa wa Benki Kuu ya Tanzania (wa kwanza kushoto) Bw. Michael Mpiri, akitoa elimu ya utambuzi wa alama za usalama katika fedha (noti) halali za kitanzania kwa wanafunzi wa shule mbalimbali mkoani Geita waliofika katik Banda la Benki kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika uwanja wa Bombambili Mkoani Geita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here