Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akimuangalia Ofisa wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Claudia Manyanda pamoja na maofisa wenzake wakati wakipanda mti alipotembelea kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita serikali inahimiza Taasisi, Mashirika pamoja na wananchi mbalimbali kupanda miti ili kutunza mazingira.
Ofisa wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Claudia Manyanda pamoja na maofisa wenzake wakifurahia jambo wakati wakipanda mti wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira alipotembelea kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi. Zahra Michuzi wakifurahia jambo pamoja na Maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania BoT mara baada ya kupanda katika viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita wakati alipotembelea kwenye maonesho hayo ya 5 ya teknolojia ya madini yanayofanyika mkoani humo.