Home LOCAL BIMA YA AFYA KWA WOTE KULETA UHAKIKA WA MATIBABU KWA WANANCHI...

BIMA YA AFYA KWA WOTE KULETA UHAKIKA WA MATIBABU KWA WANANCHI WOTE

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya, Edward Mbaga akizungumza katika atika semina kwa wahariri na waandishi wa habari juu ya sheria ya Bima ya Afya kwa wote iliyofanyika  Jijini Octoba 12,2022 Dar es Salaam.

Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Bima (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware akielezea namna ambavyo Taasisi hiyo ilivyojipanga katika kusimamia shughuli za Bima hapa nchini ikiwemo Bima ya Afya kwa wote inayotarajiwa kuanza kutolewa kwa wananchi wote.

Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya Catherine Sungura akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari alipokuwa akiwakaribisha kwenye semina hiyo.

Mjumbe wa Sekretarieti ya Mchakato wa Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote Janethi Kibambo akielezea faida mbalimbali za uwepo wa Bima hiyo alipokuwa akiwasilisha mada juu ya mapendekezo yalipo katika rasimu ya Sheria hiyo.

(PICHA NA: Hughes Dugilo)

PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI KATIKA SMINA HIYO.

Na: Hughes Dugilo, DSM

Imeelezwa kuwa uwepo wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote kutapelekea kuwepo kwa huduma bora za Afya zitakazomuwezesha kila mwananchi kupata matibabu mahali popote nhini.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya, Edward Mbaga katika semina kwa wahariri na waandishi wa habari juu ya sheria ya Bima ya Afya kwa wote iliyofanyika Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mbaga alisema kuwa Serikali imedhamiria kuimarisha huduma za Afya na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anajiunga kwa hiyari katika Bima hiyo ili kumudu gharama za matibabu pamoja na wategemezi wake.

Aidha alisesema  katika kutekeleza mpango huo Serikali itahakikisha kunakuwepo na mazingira wezeshi ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba sambamba na uwepo wa wataalamu wa kutosha katika vituo vya  afya na hospitali zote kubwa nchini.

“Bima itampa uhakika mwanachi kupata matibabu kwa haraka kwa kiwango kilekile alichochangia wakati wote pale anapokwenda katika kituo cha Afya au hospitali kubwa” alisema Mbaga.

Awali akiwasilisha mada kwa washiriki wa semina hiyo juu ya mapendekezo mbalimbali yaliyopo katika rasimu ya Sheria hiyo Mjumbe wa Sekretarieti ya Mchakato wa Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote Janethi Kibambo ameelezea faida mbalimbali za uwepo wa Bima hiyo ambapo amesema endapo sheria hiyo itapitishwa itakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wote kutokana na kuwepo wa kitita kimoja cha msingi cha matibabu.

Alisema  chini ya Sheria hiyo vitita sawa vitatolewa kwa wateja watakapokuwa wakipata huduma katika hospiotali  za umma na  za Binafsi.

Kwa upande wake Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Bima (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware alisema mamlaka hiyo imejipanga vyema kuhakikisha inasimamia na kuhakiksha huduma bora za bima ya afya  zinatolewa kwa wananchi wote.

Aidha aliwataka wanachi kuwafichua watoa huduma wanokwenda kinyume na taratibi na sheria ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.

“Tumejipanga vizuri kuhakikisha huduma za bima ya afya zinatolewa kwa viwango stahiki kwa mujibu wa sheria na kila mtanzania ananufaika na huduma bora zitakazikuwa zikitolewa katika vituo vyote vya Afya” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here