Home LOCAL

Waziri Ummy ametembelea kituo cha kutibu magonjwa ya mlipuko na ambukizi cha Temeke {Temeke Isolation Center} pamoja na Kipawa.

Ameongeza “Tuliweza kuishi na corona, ukisoma who watu 10 angalau vifo ni 40%, kwa sababu ya maendeleo ya matibabu tunaweza kuokoa watanznaia wengi.

“Hakuna chanjo ya ebola kirusi cha sudan, ila kwa aina ya Zaire chanjo ipo, hili ni jambo kubwa na gumu tuendelee kuomba isiingie kwetu.

“Lakini Wizara tunazidi kujiimarisha akitokea mgonjwa tunampeleka wapi, tusianze kuhangaika.

Ameongeza “Nimefika hapa kukutana na timu ya haraka Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza {Rapid Response Team}.

Virusi vya Ebola ni tishio kubwa zaidi kwani mtu akiambukizwa hushambulia mwili wake ikiwamo viungo muhimu ndani ya mwili wake {ini na figo} na hatimaye kifo hasa ikiwa hatapata tiba yoyote ile.

Mashambulizi hayo ya viungo ndani ya mwili ndiyo ambayo husababisha mtu kutoka damu sehemu mbalimbali za mwili wake “Si ugonjwa m-laini tuliweza kuishi na CORONA lakini si Ebola, Ebola inakulaza kitandani ni tishio,” amesema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

“Ebola ni tishio jana Waziri wa Afya wa Uganda ameniambia wamepata wagonjwa wapya 5 inafanya idadi ya waliopata maambukizi hayo tangu mlipuko {Septemba, 2022} kufikia sasa ni jumla ya watu 126.

waliolazwa {Active Cases Admitted in hospital} 54 na vifo 32 vimethibitika. Uganda kufikia sasa wanafuatilia watu 2183 {contacts} ambao walikuwa karibu na watu waliothibitishwa kuwa na ebola,” amesema.

Waziri Ummy amesema Uganda watu 38 tu ndiyo waliothibitika kupona Ebola hadi sasa.

“Wasiwasi wetu unazidi baada ya kuwa ugonjwa umeingia Kampala na Entebbe kwa hiyo ndege zinazokuja kutoka Kampala, kuja Dar es Salaam na mabasi “Kuibuka kwa Ebola Uganda kunaiweka Tanzania katika hatari ya kupata mlipuko huu Kutokana na mwingiliano mkubwa wa kiuchumi na kijamii na Uganda”.

“Tunaiona hatari kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa sababu ugonjwa tayari upo Kampala na Entebbe na Hivyo Waziri wa Afya wa Uganda ameahidi kuipa Tanzania orod.ha ya wahisiwa wa Ebola ili wasiweze kuruhusiwe kabisa kuingia Tanzania

Amesema Shirika la Afya Duniani {WHO} nalo limeahidi kuleta nchini Tanzania wataalamu ambao waliwahi kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola ikiwamo huko Liberia na kusisitiza hadi sasa Tanzania haina mgonjwa wa Ebola.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here