Home Uncategorized MADAKTARI BINGWA KUTOKA IRELAND WAPIGA KAMBI MOI

MADAKTARI BINGWA KUTOKA IRELAND WAPIGA KAMBI MOI

 Na: Mwandishi wetu, DSM.

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili –MOI imepokea jopo la madaktari bingwa wa mifupa wa watoto kutoka Taasisi ya ‘Children Health Ireland Africa’ ambapo wataendesha kambi maalum ya upasuaji kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa MOI kwa siku nne.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface amesema ujio wa madaktari bingwa kutoka Ireland ni sehemu ya mkakati wa MOI wa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za kimataifa ili kuboresha huduma kwa wananchi.

“Leo tumepokea wageni kutoka nchini Ireland ambapo watakua nasi hapa kwa siku nne ambapo watatoa huduma kwa wagonjwa ikiwemo upasuaji kwa watoto 10 wenye viungo vilivyopinda” Alisema Dkt. Boniface.

Dkt. Boniface amesema ushirikiano kati ya Taasisi ya MOI na CHIA utajikita katika maeneo ya Mafunzo , kubadilishana watumishi, utafiti, tiba mtandao pamoja na vifaa tiba.

Afisa uendeshaji Mkuu wa Shirika la ‘Children Health Ireland Africa’ Bw. Joe Gannon amesema ni heshma kubwa kupata fursa ya kushirikiana na hospitali ya MOI ili kuangalia namna bora ya kuboresha huduma kwa watoto.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya CHIA Dkt. Paula Llelly amesema ushirikiano kati ya Taasisi yake na MOI utakua na manufaa makubwa kwa pande zote mbili ambapo wanaufaika wakubwa watakuwa wagonjwa.

Katika kutekeleza kwa vitendo agizo la Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi,

Taasisi ya MOI imekua ikianzisha ushirikiano na Taasisi mbalimbali za kimataifa ili kuboresha huduma zake kwa watanzania na kumaliza rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi

Previous articleWAZIRI MKUU AWASILI KOREA KUSINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Next articleWATOA HUDUMA ZA AFYA 3000 KUPEWA MAFUNZO KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA- PROF. RUGGAJO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here