Home BUSINESS WAZIRI WA MADINI DK. BITEKO AIPONGEZA NSSF KWA KUYAFIKIA MAKUNDI MBALIMBALI

WAZIRI WA MADINI DK. BITEKO AIPONGEZA NSSF KWA KUYAFIKIA MAKUNDI MBALIMBALI

Waziri wa Madini,Mhe. Dotto Biteko leo tarehe 1 Oktoba ,2022 ametembelea banda la NSSF katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya uwekezaji (EPZA) Bombambili Mkoani Geita.

Ambapo aliupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unavyohakikisha unatekeleza mpango wake wa kuyafikia makundi mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogowadogo wa madini katika maeneo mbalimbali.

NSSF inashiriki Maonesho hayo kwa lengo la kutoa huduma mbalimbali za Hifadhi ya Jamii kwa wanachama na wananchi ikiwa pamoja na kusajili wanachama wapya wanaofika katika Banda la NSSF.

Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF,Lulu Mengele akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini ,Mhe.Dotto Biteko leo 1 Oktoba,2022 wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya uwekezaji (EPZA)Bombambili Mkoani Geita.

Waziri wa Madini,Mhe. Dotto Biteko akisasaini kitabu cha wageni mara baaada ya kumaliza ziara yake fupi katika Banda hilo.

Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akiwa Katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mfuko wa NSSSF alipotenbelea na kusaini kitabu Cha wageni katika kanda Hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here