Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko na Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen wakikata keki wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Na: Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameongoza Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Redio ya Kibiashara inayomilikiwa na Kampuni ya Neptune Media Ltd ya Gold Fm (Gold Fm 1st Anniversary) zilizofanyika Septemba 2,2022 katika Klabu ya Magic 101 Mjini Kahama
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kwa Niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye , Dkt. Biteko ameipongeza Gold Fm kwa kwa kazi nzuri wanayoifanya kuihabarisha jamii na kutangaza madini ya dhahabu kupitia jina lake (Gold Fm).
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema ameishukuru na kuipongeza Gold Fm kwa namna inavyoshirikiana na serikali katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amekubali ombi la Mkurugenzi huyo wa Gold Fm Neema Mghen aliloomba kuwa mwaka ujao wa 2023 wawasilishe ombi la kibali cha kusikika mikoa 10 hasa wakianzia na mikoa ya Kanda ya ziwa.
“Nawapongeza Gold Fm kwa kuendelea kufanya vizuri, na hata lile ombi lenu la kutaka msikike kwenye mikoa 10 tumelikubali. Milango ipo wazi hata mkitaka leo, Kibali kipo wazi njooni hata leo”,amesema Mihayo.
Mhandisi Mihayo ametumia fursa hiyo kutoa elimu kuhusu Kampeni ya Kwea Kidijitali kwa kuhamasisha wananchi kufanya uhakiki wa usajili wa laini ya simu kwa kupiga *106#, Matumizi sahihi ya namba 100 matumizi ya namba 15040 endapo watapigiwa simu au kupata ujumbe wa kitapeli huku akiwasisitiza wananchi kuzingatia Matumizi salama ya mtandao kwa ajili ya Maendeleo ya Uchumi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm, Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen amesema katika kipindi cha mwaka mmoja, Gold Fm imekuwa redio pendwa katika ukanda wa Ziwa kutokana na namna yake bora ya utoaji wa maudhui, umahiri wa Watangazaji wake na utoaji wa taarifa zenye ukweli, kwa wakati na zinazozingatia Mizania.
“Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Redio yetu imekuwa pendwa kutokana na vipindi vyake kujikita zaidi katika Masuala ya Kijamii, Habari na Burudani, na hivyo kufanikiwa kuwa mshindi wa Tuzo nne kati ya tano wa Watangazaji bora mwaka huu, zilizotolewa na Taasisi ya Holly smile”,amesema Neema.
Ameeleza kuwa katika kipindi cha Mwaka mmoja Gold Fm imefanikiwa kufanya matukio mbalimbali makubwa ikiwemo kudhamini na kusimamia ligi ya Taifa ngazi ya Mkoa wa Shinyanga, Ligi ya mabingwa wa Mikoa ambayo ilishirikisha mikoa 7 na kwa sasa wanaendelea na Ligi ya wilaya ya Kahama ambayo inashirikisha timu 32.
“Mbali ya matukio hayo ya kimichezo, pia tumefanya matamasha mbalimbali ya muziki pamoja na kuiunga mkono serikali katika matukio mbalimbali ikiwemo Uhamisishaji wa zoezi la Anuani za makazi, Uchangiaji Damu, Sensa ya watu na makazi, mwenge wa uhuru, chanjo ya UVIKO 19, Maadhimisho ya siku ya wanawake na mengine mengi ambayo kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja yametuongezea usikilizwaji wa redio yetu katika maeneo yote ya mkoa wa Shinyanga na baadhi ya mikoa Jirani”,ameeleza.
“Mheshimiwa Mgeni Rasmi kama ilivyo kila kwenye mafanikio hapakosi changamoto, katika mwaka huu mmoja tulikuwa na changamoto kubwa ya masafa yetu kuwafikia wasikilizaji wetu wote wa mkoa wa Shinyanga kutokana na Jiografia ya mkoa huu kwa kuwa mitambo yetu ya matangazo ipo Kahama hivyo kufikia vizuri wasikilizaji wa Shinyanga mjini ilikuwa changamoto.
Hata hivyo Mheshimiwa Mgeni Rasmi ninayo furaha kukueleza hapa pamoja na wana Shinyanga kwa ujumla kuwa Tayari tumepata kibali kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA cha kuongeza mitambo ya matangazo na kusikika katika mkoa mzima ambapo tumefunga pale Kilulu, Tinde na sasa wasikilizaji wa Shinyanga Mjini akiwemo mkuu wetu wa mkoa hapa wanatusikia vizuri kupitia masafa yetu ya 88.7”, amefafanua.
Hata hivyo Mghen amesema katika kuendelea kuwa chombo bora cha Habari Kanda ya ziwa na hata Tanzania, Gold FM itazidi kuzingatia misingi ya Habari kwa kuzingatia weledi wakati wote na pia kuhakikisha wanajikita kwenye Habari za uchunguzi.
“Mafanikio yote haya yamechagizwa na ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Kanda ya ziwa, viongozi wa serikali wilaya ya Kahama, viongozi wa serikali mkoa wa Shinyanga, Taasisi za serikali, taasisi binafsi, taasisi za dini, Wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla “nawashukuru sana”, amesema.
“ Gold FM kama chombo cha Habari ambacho watendaji wake ni waandishi wa Habari, tunafahamu nia njema ya serikali kupitia Idara ya Habari Maelezo kuelekeza waandishi wa Habari kuwa na Press card ili kutambulika, lakini kumekuwa na changamoto ya wanahabari kutakiwa kukata Press card kila mwaka na wakikata zinachelewa kutoka, hivyo tunaiomba serikali iangalie uwezekano wa Press card kuwa za angalau muda wa miaka mitano na ziwe za kielektroniki”,amesema.
Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm yamepambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Khadija Kopa na Christian Bella.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim.
Mkurugenzi wa Klabu ya Magic 101 , Emmanuel Peter Kabakezi akizungumza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko na Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen wakikata keki wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akikata keki wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm. Kushoto ni Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen.
Wafanyakazi wa Gold Fm,
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Edwin Dellah ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Maadhimisho ya mwaka mmoja wa Gold fm akielezea huduma wanazotoa.
Msanii Christian Bella akitoa burudani wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Msanii Christian Bella akitoa burudani wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Msanii Khadija Kopa akitoa burudani wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Msanii Khadija Kopa akitoa burudani wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Msanii Khadija Kopa akitoa burudani wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akimtunza msanii Khadija Kopa.
Msanii Khadija Kopa akitoa burudani wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.
Msanii Khadija Kopa akitoa burudani wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Gold Fm.