Home LOCAL WATAKAOSALIMISHA SILAHA WANAZOMILIKI KINYUME CHA SHERIA KUSAMEHEWA

WATAKAOSALIMISHA SILAHA WANAZOMILIKI KINYUME CHA SHERIA KUSAMEHEWA

Na:Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi linapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa,kutakuwa na uzinduzi wa kampeni maalum ya mwezi mmoja unaojulikana kama msamaha wa Afrika itakayohusisha usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari zinazomilikiwa na baadhi ya watu kinyume cha sheria, ama kwa kutokujua taratibu za kisheria za umiliki wa silaha.

Akitoa taarifa hiyo leo septemba 03 2022 msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP-DAVID MISIME amesema Uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika tarehe 05.09.2022 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika viwanja vya mashujaa mkoa Dodoma,ambapo Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (MB).

Aidha Misime amesema baada ya uzinduzi huo tushirikiane sote kuelimishana wananchi kuwa yeyote atakayesalimisha silaha anayo miliki kinyume cha sheria katika muda utakaotolewa na Mhe.Waziri siku hiyo, hatochukuliwa hatua yeyote ile.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here