Na Lucas Raphael,Tabora
Watu watano wakiwemo wanne waliokamatwa kwa tuhuma za kuwaua askali wawili wa jeshi la Polisi kituo cha Usoke Wilayni Urambo mkoani Tabora wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani na Mahakama kuu kanda ya Tabora.
Adhabu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora aliyekasimiwa Mamlaka ya Ziada Jovin Katto baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Mashitaka.
Waliopea adhabu hiyo katika kesi ya kwanza ni Shedrack Hamis Rushikama, Sylvesta Mussa Kingwendu, Abel Benedict na Ramadhani Kassim Manywele ambao walikuwa wakikabiliwa na mashita mawili ya mauaji na Unyanganyi wa kutumia silaha.
Alisema kwamba mahakama pasipo shaka yoyote imeweza kuwatia hatiani washitakiwa hao baada ya kupata ushaidi usiotia shaka .
Hakimu hiyo aliendelea kusema kwamba kutokana na baadhi ya watu kuamua kujichukua sheria mikononi hivyo ni fundisho kwa kila moja ambaye anatumia nguvu kuporoa ama kuua kwa kutoa uhai wa mtu jambo ambalo linapingana na sheria za nchini.
Awali Upande wa mashitaka ukiongozwa na Mawakili Meroto Ukongoji na Tunosye Luketa uliiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo mnamo Aprili 28/2014 majira ya usiku eneo la Ussoke.
Uliongeza kusema kwamba siku hiyo washitakiwa walimuuwa Askali polisi wenye namba G3388 pc Shabani Mbua na namba G 4602 kwa kuwapiga risasi.
Askari hao wawili waliuwawa wakati wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi na usalama kwenye kituo cha Polisi Usoke wilayani Urambo mkoani Tabora mwaka 2014
Akitoa uamzi huo Hakimu Alipewa mamlaka ya ziada Jovin Katto alisema mahakama imewatia hatiani kwa makosa hayo hivyo inawahukumu kunyongwa hadi kufa lakini wanaruhusiwa kukata rufaa kama hawakuridhika na adhabu hiyo.
Upande wa utetezi katika shauri hilo ulikuwa unawakilishwa na mawakili Fravian Fransisi, Amos Gaise Chistina Jacson na Chales Hayo.
Katika shauri lingine mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora imemhukumu kunyongwa hadi kufa Nelson Maige baada ya kumtia hatiani kwa kumuua Mkewe kwa kutumia kitu chenye ncha kali kutokana na wivu wa Mapenzi.
Upande wa Mashitaka uliiambia mahakama hiyo kuwa oktoba 12/2019 katika kijiji cha Loya Wilaya ya Uyui mkoani Hapa Mshitakiwa alimua Mkewe aitwaye Vailet kwa kumchoma kisu Shingoni.