Home LOCAL WADAU WA HABARI NCHINI WATAKIWA KUJIPANGA WATAKAPOITWA NA KAMATI HUSIKA KUTETEA MAPENDEKEZO...

WADAU WA HABARI NCHINI WATAKIWA KUJIPANGA WATAKAPOITWA NA KAMATI HUSIKA KUTETEA MAPENDEKEZO YA MABADLIKO YA SHERIA YA HABARI

Kauli hiyo imetolewa na Dk. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Ubungo alipozungumza na mwandishi bungeni jijini Dodoma kuhusu mchakato wa mabadiliko ya sheria hiyo iliyotungwa mwaka 2016.

Dk. Kitila amesema, kwa kawaida wadau wa habari watakutana na kati na kule ndio wanapaswa kueleza hoja zao kwanini wanadhani baadhi ya vifungu hivyo vinapaswa kubadilishwa.

“Wadau wa habari kujipanga ili watakapokuja kwenye kamati husika waweze kutoa hoja zao kwanini wanataka baadhi ya vifungu katika Sheria ya Huduma za Habari 2016 viboreshwe.

“Unafahamu kwenye kamati ndio wadau wanapata nafasi ya kutoa hoja zao kwanini wanataka baadhi ya vipengele vifanyiwe marekebisho,” amesema Prof. Kitila.

Akizungumzia mchakato huo Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) amesema, ingawa mpaka sasa hajajua wakati ambao maoendekezo hayo yatafikishwa bungeni, lakini bado ana matumaini kwamba safari ya mabadiliko hayo haitaishia njiani.

Balile amesema, serikali bado inaonesha kuwa na dhamira njema ya kufanya mabadiliko.

“Waziri wa Habari ndiye mwenye kujua lini watapeleka bungeni muswada lakini sisi wadau tumepewa fursa ya kutoa maoni yetu.

“Tumeona dhamira njema ya serikali hadi hivi sasa, tukiendelea hivi nadhani huko tuendako tutashirikiana vizuri kwa masilahi ya Taifa letu,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here