Mkurugenzi wa kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Hexad Bw. Fortnatus Luhemeja akitoa maelezo kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw. Geofrey Meena wakati alipotembelea mgodi huo kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa mgodini hapo.
Mgodi wa Hexad ni miongozi mwa wanufaika wa kituo cha Mfano cha Uchenjuaji madini cha Rwamgasa mkoani Geita kinachowasaidia wachimaji wadogo wa dhahabu ambapo STAMICO iliandaa ziara ya wadau mbalimbali kutembelea mgodi wa Buckreef Gold Limited na hituo hicho cha Rwamgasa kinachomilikiwa na STAMICO ikiwa ni muendelezo wa maonesho ya tano ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.
(PICHA ZOTE NA: JOHN BUKUKU) Fullshangwe Blog.
GEITA.
Imeelezwa kuwa kutokana na huduma inayotolewa na Kituo cha mfano cha uchenjuaji wa dhahabu kinachomilikiwa na Shirika la Madini la Tanzania STAMICO cha Rwamgasa kimerahisisha na kuongeza thamani ya Kampuni wachimbaji wadogo inayojishughulisha na uchimbaji wa Madini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hexad inayojishughulisha na uchimbaji wa Madini Bw. Fortnatus Luhemeja wakati akizungumza katika Kituo cha mfano cha uchenjuaji wa dhahabu kinachomilikiwa na STAMICO katika kijiji cha Rwamgasa mkoani Geita.
Amesema kituo hicho kimeongeza thamani kubwa kwenye shughuli zake za uchimbaji wa madini kutokana na kutoa huduma ya CIP ambapo imesaidia kupeleka mawe yao kwa muda mfupi na kuweza kupatiwa dhahabu kutoka kwenye mawe hayo.
Luhemeja ameeleza kuwa awali walikuwa wakitumia mfumo wa mekiuri ilikuwa inachukua asilimia 25 kwa mekiuri na Vatilishin ilikuwa inachukua 75 hivyo kituo hicho kinachukua asilimia 95 mpaka 97 jambo ambalo limewahakikisha upatikanaji wa dhahabu kwa urahisi.
Amesema eneo hilo limekuwa na historia ya kutumika kabla hata ya uhuru hivyo mpaka sasa wamechimba mpaka mita 76 wakiitafuta dhahabu jambo ambalo inawapa tija na mafanikio.
‘Uzuri ni kwamba PPM 5 tunayoipata tunaweza tukaipata dhahabu kwa muda mfupi na maana ya hii PPM 5 ni wingi wa dhabau kwenye yale mawe yaliyopo ndani’amesema Luhemeja
Aidha akizungumzia kuhusiana na Shirika la STAMICO amesema kuwa linawasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapatia mafunzo ya mfano ya mara kwa mara ili kurahisisha shughuli zao.
Amesema kupitia maonyesho ya Madini yanayoendelea STAMICO inawaonyesha namna ambavyo teknolojia inatumika katika masuala ya uchimbaji wa madini.
STAMICO imeendelea kuwa mlezi wa wachimbaji wadogo ili hatimaye waweze kukua na kuongeza tija katika kufanya shughuli zao.
Mkurugenzi wa kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Hexad Bw. Fortnatus Luhemeja akitoa maelezo kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw. Geofrey Meena wakati alipotembelea mgodi huo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Hexad Bw. Fortnatus Luhemeja akitoa maelezo kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw. Geofrey Meena katika moja ya shimo la mgodi huo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Hexad Bw. Fortnatus Luhemeja akihojiwa na waandishi wa habari na kuelezea jinsi kituo cha mfano cha Rwamgasa kinavyowasaidia katika kuchenjua dhahabu.
Moja ya mashine za kusaga mawe katika mgodi wa Hexad uliopo Rwamgasa.
Mkurugenzi wa kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Hexad Bw. Fortnatus Luhemeja akiongozana na Meneja Masoko na Uhusiano wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw. Geofrey Meena wakati akitembelea mgodi huo.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw. Geofrey Meena akielekeza jambo kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Hexad Bw. Fortnatus Luhemeja wakati alipotembelea katika mgodi huo.
Wadau mbalimbali wakitembelea katika kituo cha mfano cha kuchenjua dhahabu cha Rwamgasa.
Bw. Victor Oral Msimamizi wa Kituo cha Mfano cha Uchenjuaji wa Dahabu Rwamgasa akitoa maelezo kwa wadau mbalimbali waliotembelea katika kituo hicho ili kuona namna kinavyowasaidia wachimbaji wadogo wa dhahabu.
Mkurugenzi wa kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Hexad Bw. Fortnatus Luhemeja mchimaji mdogo wa dhahabu ambaye amenufaika na kituo cha mfano cha Rwamgasa akitoa ushuhuda wake kwa wadau waliotembelea katika kituo hicho.
Moja ya mashine za uchorongaji zinazofanya utafiti katika mgodi wa Buckreef Gold Limited ikiendelea na kazi ya uchorongaji.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw. Geofrey Meena akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa STAMICO na mgodi wa Buckreef Gold Limited kushoto ni Bibiana Ndumbaro Afisa Masoko na Uhusiano STAMICO.
Mhandisi Mwandamizi wa Mgodi wa Buckreef Gold Limited akitoa maelezo kwa wadau waliotembelea katika mgodi huo.
Wadau mbalimbali waliotembelea katika mgodi wa Buckreef Gold Limited wakipata maelezo kuhusu mtambo mpya unaofungwa katika mgodi huo kwa ajili ya kuchenjua dhahabu.
Picha ya pamoja katika kituo cha mfano cha kuchenjua dhahabu cha Rwamgasa.