Home BUSINESS WACHIMBAJI WADOGO MSITUMIE WAGANGA WA JADI KWENYE UCHIMBAJI WA MADINI

WACHIMBAJI WADOGO MSITUMIE WAGANGA WA JADI KWENYE UCHIMBAJI WA MADINI

Na. Costantine James, Geita.

Wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Geita wametakiwa kuachana na imani potofu yakwenda kwa waganga wa jadi kuchinja kuku katika maduara kwa lengo la kubaini madini yalipo.

Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa Madini Tanzania(GST) Mkoa wa Geita John D. Kalimenze amesema kuna baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wanatumia wanganga wa jadi katika shughuli za uchimbaji wa madini kwa lengo la kubaini madini yalipo.

Amewataka kuachana na imani hizo za kishirikina kwa kuhusisha waganga wa jadi katika kubaini sehemu madini yalipo na Badala yake watumie teknolojia ya Kisasa kwa kupeleka Sampuli Maabara za kisasa ili kubaini uwepo wa madini katika sehemu husika.

Amesema imani za kishirikina zina athali kubwa kwa wachimbaji wadogo kwani maranyingi wamekuwa wakipoteza pesa pamoja na mda kuchimba madini katika sehemu ambayo hayapo baada ya kutumia waganga wa jadi katika kubaini madini yalipo.

Nao baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini waliojitokeza katika Maonesho ya tano ya Kitaifa ya teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili Mkoani Geita wamekiri kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kutambua sehemu madini yalipo.

Previous articleUPATIKANAJI WA HUDUMA ZA BRELA KWA NJIA YA MTANDAO UMERAHISISHA WANANCHI KURASIMISHA BIASHARA ZAO
Next articleTANZANIA, INDIA KUONGEZA USHIRIKIANO SEKTA YA FILAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here