Home BUSINESS WACHIMBAJI WA MADINI WATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA

WACHIMBAJI WA MADINI WATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA

Mkuu wa Wilaya ya Nyangh’wale Jamhuri David (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mazingira wa Tume ya Madini Hyasinta Laurean (wa nne kutoka kushoto) mara baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kufika katika Banda la Taasisi hiyo kuona shughuli mbalimbali wanazozifanya kwenye Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Nyangh’wale Jamhuri David (kulia) akifurahia jambo alipokuwa akipokea maelezo kutoka kwa Afisa Mazingira wa Tume ya Madini Hyasinta Laurean (kushoto) wakati wa ziara ya Mgeni huyo katika banda la Taasisi hiyo.

Maafisa wa Tume ya Madini wakimsikiliza Mkuu Mkuu wa Wilaya ya Nyangh’wale Jamhuri David (hayumo pichani) wakati Mgeni huyo alipofika kwenye Banda lao kuwatembelea.

Na: Costantine Jmes, Geita.

Wachimbaji wa madini Mkoani Geita wametikiwa kutunza mazingira wakati washughuli za uchimbaji wa madini kwa lengo la kulinda na kuhifadhi mazingira.

Hayo yamebainishwa na tume ya madini Tanzania katika Maonesho ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya Madini 2022 yanayofanyika kitaifa Viwanja vya EPZA Bombambili Mkoani Geita.

Afisa mazingira kutoka tume ya madini Hyasinta Laurean amesema utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mtu hivyo wachimbaji wa madini ni moja ya kundi mhimu linalopaswa kuzingatia zaidi sheria na kanuni za utunzaji wa mazingira.

Amesema Shughuli uchimbaji wa madini zinachangia kwa kiasi katika uhalibifu wa mazingira hivyo wachimbaji wanapokuwa wanachimba madini au wakati wa uchenjuaji wanapaswa kuzingatia utunzaji wa mazingira katika sehemu wanayofanyia kazi.

Kutokana na Shughuli za uchimbaji wa madini kwa kiasi kikubwa kuwa na matumizi ya kemikali mbalimbali wanazozitumia katika uchenjuaji wa madini hivyo wanapaswa kuzingati vyema matumizi ya kemikali hizo ili zisiwe chanzo cha uhalibifu wa mazingira.

Amewataka wachimbaji kufanya kazi zao katika mazingira ya usalama ikiwa ni pamoja na kufata sheria na taratibu za mazingira kwa lengo la kuyaweka mazingira katika hali ya usalama.

Amewataka wachimbaji kushiriki vyema katika maonesho hayo pamoja na kutembelea banda la tume ya madini ili kujipatia elimu zaidi juu ya uchimbaji wa madini pamoja na utunzaji wa mazingira.

“watu wanaojishughulisha na waliowekeza katika madini wanatakiwa wajikinge na walinde mazingira yao yanayowazunguka hasa maeneo wanayofanyia kazi ili kutunza mazingira “ Amesema Hyasinta Laurean.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here