Home BUSINESS TEITI YATOA ELIMU KWA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA

TEITI YATOA ELIMU KWA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA

Mkuu wa Wilaya ya Nyanh’wale David William (kulia) akisiliza maelezo kutoka kwa Afisa Msimamizi wa Fedha wa Taasisi  ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Erick Ketagory (wa kwanza kushoto) wakati mgeni huyo alipokuwa kwenye Banda la Taasisi hiyo kuona shughuli wanazofanya.
Mkuu wa Wilaya ya Nyanh’wale David William  (kulia) akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kumaliza kutembelea kwenye Banda hilo.
Afisa Msimamizi wa Fedha wa Taasisi  ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Erick Ketagory akitoa elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Taasisi hiyo.

Na: Hughes Dugilo, GEITA

Taasisi  ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) ni Taasisi iliyodhamiria kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uelewa wa namna  inavyotimiza majukumu yake ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,Mafuta na Gesi Asilia kwa mujibu wa Sheria.

Majukumu wanayoyasimamia kwa mujibu wa Sheria, ni pamoja na kuweka wazi taarifa za Mapato ya Serikali na malipo ya Kodi yanayotoka kwenye Kampuni za Madini,Mafuta na Gesi Asilia kwa Umma ili kuhamasisha  Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali hizo.

Ndio maana TEITI wameamua kushiriki kwenye Maonesho ya tano ya Teknolojia ya Sekta ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita ili kukutana na wananchi moja kwa moja na kuzungumza nao kwa kuwapa elimu juu ya kazi zinazotekelezwa na Taasisi hiyo.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nyanh’wale David William aliyetembelea katika Banda la TEITI kwenye Maonesho hayo, Afisa Msimamizi wa Fedha wa Taasisi hiyo Erick Ketagory amesema kuwa wananchi wana haki ya msingi kwa mujibu wa Sheria kupata taarifa zote muhimu za Mapato ya Serikali na malipo ya Kodi yanayotoka kwenye Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia.

“Taasisi hii ina wajibu mkubwa wa kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Ndio maana sisi tuko hapa kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu kuwa wanao wajibu wa kupata taarifa hizi kwa usahihi” ameeleza Ketagory.

Taasisi hiyo imeundwa kwa Sheria namba 23 ya TEITA ya mwaka 2015 ambayo imeunda Kamati ya Uwazi na Uwajibikaji (Kamati ya TEITI) yenye wajumbe nane(8) inayoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu Ludovick Utouh ambapo kazi za kila siku za TEITI zinatekelezwa na Katibu Mtendaji.

 

Previous articleSERIALI INAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NCHINI: DKT. KIJAJI
Next articleMAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 30-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here