Home SPORTS SMZ KUSHIRIKIANA NA TANZANIA BARA KUKUZA MICHEZO

SMZ KUSHIRIKIANA NA TANZANIA BARA KUKUZA MICHEZO

NA: FARIDA MANGUBE. MOROGORO.
Waziri wa habari , vijana , utamaduni na micheza wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar mheshimiwa Tabia Mauled Mwita, amewataka wakurugenzi wa mashirika yanayoshiriki mashindano ya michezo ya bandari (Interport games) kuona uwezekano kwa mashindano ya mwaka 2023 kufanyika visiwani zanzibar kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi, umoja wa kitaifa na kudumisha muungano.
Waziri Mwita ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifungua mashindano ya 16 ya michezo ya bandari (Interport games) ambapo amesema wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Wizara ya utamaduni sanaa na michezo ya jamuhuri ya uungano wa Tanzania zimejipanga vyema kuhakikisha zinasimamia ipasavyo sekta ya michezo kwa pamoja ili kuleta ushindani katika michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
“Niwatake washiriki wote mliopata fursa kushiriki mashindano haya mwende mkashindane na kuhakikisha mnafanya vinzuri na kupata ushindi wa pamoja, lakini vilevile kuna usemi unasema kushinda au kushindwa sio kitu cha msingi sana bali kikubwa kwenye mashindano haya ni kudumisha upendo,ushirikiano na umoja kwani sisi sote ni ndugu kwaiyo michezo hii isije kupelekea kutugawa badala yake tuendelee kuimarisha mmungano wetu .” Alisema waziri Mwita.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mashindano hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya bandari nchini TPA Plasduce Mbossa, Naibu Mkurugenzi Mkuu Bwana Juma Kijavala alisema TPA inatambua umuhimu wa michezo katika kuimarisha afya za wafanyakazi kwani mfanyakazi anapokuwa na afya njema hata utendaji wake wa kazi unaimarika.
“Ni sisitize tu kwa wafanyakazi wetu wote ni vyema kufanya mazoezi hata kama hakuna michezo hii ya interport.” Alisisitiza Bwna Kijavala.
Alisema lengo la michezo hiyo ni kuongeza tija kwenye michezo ambapo aliwataka waamuzi wa michezo hiyo kutopendelea timu yoyote kwa masilahi binafsi kwani kufanya hivyo ni utovu wa nidham.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA Bi. Marim Mkama ameiomba serikali kuona kuwezekano wa mashindano hayo kufanyika mara mbili kwa mwaka ili kuongeza chachu ya ushindani kwa wanamichezo.
Mashindano hayo ambao yanafanyika kila mwaka na kwamba kwa mwaka huu yameshirikisha Taasisi nne za bandari zikiwa na timu tano ambazo zitacheza mpira wa miguu, mchezo wa kamba, riadha, pamoja na mpira wa kikapu.
Previous articleUBORESHAJI WA SHERIA YA USALAMA BARABARANI UTASAIDIA KUPUNGUZA VIFO VYA VINAVYOTOKANA NA AJALI
Next articleKAMATI YA BUNGE YAISHAURI SERIKALI KUREJESHA USIMAMIZI WA MASUALA YA CHAKULA KWA TMDA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here