Home BUSINESS NHC YAJA NA MRADI WA ‘SAMIA HOUSING SCHEME’ KWAAJILI YA MAKAZI

NHC YAJA NA MRADI WA ‘SAMIA HOUSING SCHEME’ KWAAJILI YA MAKAZI

Mounekano wa nyumba mbalimbali katika picha zitakazojengwa kwenye mradi wa Samia Housing Scheme Kawe jijini Dar es Salaam.

Afisa Mauzo na Masoko Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Daniel Kure akitoa maelezo kuhusu mradi wa Samia Housing Scheme unaojengwa Kawe katika jiji la Dar es Salaam kwenye maonesho ya tano ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika EPZA Bombambili mkoani Geita.

Afisa habari Shirikala Nyumba la Taifa (NHC) Domina Rwemanyila akitoa maelezo kuhusu mradi wa Samia Housing Scheme unaojengwa Kawe katika jiji la Dar es Salaam kwenye maonesho ya tano ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika EPZA Bombambili mkoani Geita.

Afisa habari wa NHC Domina Rwemanyila akifafanua jambo kwa mnufaika wa mradi wa nyumba za NHC  Bombambili zilizopo Mkoani Geita Bw. Andrew Mwinuka,  alipotembelea katika Banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya madini mjini Geita.

Afisa Mauzo na Masoko Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Daniel Kure (kulia) na Afisa habari wa Shirika hilo Bi. Domina Rwemanyila wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la Taasisi hiyo.

(PICHA NA HUGHES DUGILO)

 Na: Mwandishi wetu, GEITA.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Limekuja na mradi wa ujenzi wa nyumba unaojulikana kama Samia Housing Scheme unaolenga kujenga nyumba za makazi nchi nzima kwa ajili ya makazi kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mauzo na Masoko mwandamizi kutoka Shirika la nyumba la Taifa (NHC) Daniel Kure wakati akizungumza na wandishi wa habari katika Maonesho ya tano ya kitaifa yaTeknolojia ya Madini Mkoani Geita ambapo amesema mradi huo utatekelezwa nchi nzima na utaanzia Jijini Dar es salaam katika eneo la Tanganyika Peckers na Badae katika Jiji la Dodoma.

“Mradi huu utatekelezwa kwa awamu, ambapo utahusisha ujenzi wa nyumba za makazi nchi nzima katika maeneo mbalimbali ajili ya makazi kwa wananchi wote wenye kipato cha kati na cha chini” amesema Kure.

Ameongeza kuwa kupitia mradi huo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kujenga nyumba elfu tano katika maeneo mbalimbali kwenye mikoa yote hapa nchini.

“Utekelezaji wa mradi huu hadi utakapokamilika unatarajiwa Kughalimu Shilingi Bilioni 466 ambapo nyumba hizo zitawanufaisha watanzania wengi wenye kipato cha chini, lakini pia wale wa kipato cha kati na juu”ameongeza

Amesema katika utekelezaji wa mradi huu utawezesha kuzalisha ajira zaidi ya elf 26 kwa wantanzania katika mikoa yote wakati mradi huo utakapokuwa unatekelezwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here