Home LOCAL SERIKALI: MABADILIKO SHERIA YA HABARI IKO PALELE

SERIKALI: MABADILIKO SHERIA YA HABARI IKO PALELE

WADAU wa habari nchini, wametakiwa kuwa na subiri wakati serikali ikiendelea na mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari.

Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza na mwandishi wa habari hii amesema, serikali ipo katika hatua nzuri na kwamba, mchakato huo bado unaendelea na haujakwama.

Msigwa alitoa maelezo hayo baada ya mwaishi kutaka kujua kinachoendelea kuhusu mchakato huo, hasa baada ya kufanyika kikao kati ya serikali na wadau wa serikali tarehe 11-12 Agosti mwaka huu.

Msigwa alimweleza mwandishi “mtapewa taarifa lakini mpaka sasa, mchakato ndani ya serikali unakwenda vizuri,” alisema Msigwa ambaye amesisitiza kwamba ‘mtajulishwa.”
Awali mwanidhi alimtafuta Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akitaka kujua maendeleo ya mchakato huo.

Nape alimtaka mwandishi kuwasiliana na Msigwa, “mtafute Msigwa, huyo atakupa ufafanuzi vizuri,” alisema.

Akizungumza mwisho mwa Agosti mwaka huu, Nape alisema kikao cha wadau wa habari na serikali kiliafikiana baadhi ya vipengele vya sheria ya habarinna kwamba, kitaitishwa kikao kingine ili kufikia muafaka.

Pia alisema kuwa, serikali haitapeleka mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya habari bungeni, mpaka wadau wakubaliane kwa pamoja.

“Tunataka sheria tutakayoitunga iishi kwa muda mrefu, hatutaki tupitishe sheria halafu muda mchache tukutane tena kuirekebisha,” alisema Nape wakati akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here