Home LOCAL RUTO ASHINDA KESI MATOKEO YA URAIS KENYA

RUTO ASHINDA KESI MATOKEO YA URAIS KENYA

NAIROBI.

Mahakama ya Juu nchini Kenya imemthibitisha William Ruto kuwa ndiye mshindi wa Uchaguzi wa kiti cha  uchaguzi Mkuu  uliofanyika Agosti 09, 2022, nchini humo dhidi ya mpinzani wake wa karibu Raila Odinga aliyefungua kesi hiyo kupinga ushindi wa William Ruto.

Mahakama hiyo imesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unaoweza kubatilisha matokeo ya Urais yaliyompa ushindi William Ruto kutoka muungano wa Kenya Kwanza.

Kufuatia hali hiyo, Mahakama hiyo imesema Ruto ni Rais Mteule halali wa Taifa hilo, hivyo taratibu nyingine zinaweza kuendelea.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mkuu wa Kenya, Martha Koome amesema uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Kenya Agosti 9 mwaka huu ulikua huru na haki.

Akisoma hukumu ya kesi hiyo iliyosikilizwa na majaii saba, Jaji Mkuu Koome amesema tuhuma kuhusu taarifa za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) zilidukuliwa hazina uthibitisho wowote.

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya Urais nchini Kenya ilifunguliwa na Raila Odinga aliyekuwa mgombea urais kupitia muungano wa Azimio la Umoja na mgombea mwenza wake Martha Karua.

Wawili hao walifungua kesi hiyo ya kupinga matokeo ya urais yaliyotangazwa Agosti 15 mwaka huu na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) Wafula Chebukati, huku wakidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu katika mchakato wa uchaguzi huo, hivyo matokeo hayo ya Urais ni batili.

Previous articleBRELA YASHAURIWA KUSAIDIA WAFANYABIASHARA MKOANI MARA
Next articleBARRICK NORTH MARA YAANDAA LIGI YA SOKA YA ‘MAHUSIANO CUP’ TARIME
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here