Home BUSINESS RC MAKALLA ARIDHISHWA NA KASI YA MABORESHO NA UJENZI SOKO JIPYA LA...

RC MAKALLA ARIDHISHWA NA KASI YA MABORESHO NA UJENZI SOKO JIPYA LA KARIAKOO

 – Amshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa wakati.

– Ujenzi umefikia Asilimia 40 na Mkandarasi yupo ndani ya Muda.

– Asema maandalizi ya Mpango wa Kariakoo kufanya Biashara saa 24 yanaendelea vizuri.

Na; James Lyatuu, DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemuelekeza Mkandarasi wa Kampuni ya Estim Construction Ltd kuongeza Kasi ya Ujenzi na Maboresho ya Soko la Kariakoo likamilike kwa wakati ili Nia njema ya Rais Samia Suluhu Hassan kuona Wafanyabiashara wa Kariakoo wanafanya biashara katika mazingira Bora inatimia.

RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa Soko lililoungua na Soko jipya lenye urefu wa gorofa 6 ambapo Ujenzi unaghahirimu zaidi ya Shilingi Bilioni 26.

Katika Ziara hiyo RC Makalla ameonyesha kuridhishwa na Kasi ya Mkandarasi ambae mpaka Sasa amefikia Asilimia 40 jambo linloleta matumaini ya Soko kukamilika kwa wakati.

Aidha RC Makalla amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa kwa wakati jambo linalomuwezesha Mkandarasi kutekeleza Majukumu yake pasipo usumbufu wowote.

Pamoja na hayo RC Makalla amesema kukamilika kwa Soko Hilo itabadili mfumo wa uendeshaji biashara kwa kutoa Wigo mpana wa kupokea Wafanyabiashara wengi Zaidi kutoka Wafanyabiashara 600 mpaka kufikia Wafanyabiashara zaidi ya 2,000.

Kuhusu suala la Kariakoo kufanya biashara saa 24 Kama Rais Samia alivyoelekeza, RC Makalla amesema kikosi kazi kinaendelea kufanya tathimini Kisha kitawasilisha taarifa kwaajili ya utekelezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here