Home BUSINESS RC MAKALLA AMALIZA SINTOFAHAMU YA MABASI YANAYOTUMIA  STENDI BINAFSI

RC MAKALLA AMALIZA SINTOFAHAMU YA MABASI YANAYOTUMIA  STENDI BINAFSI

PICHA NA: MAKTABA

– Awataka LATRA kutokwepa majukumu Na nyaraka zao walizotoa kwa stendi binafsi.

– Aruhusu stendi binafsi 5 zilizohakikiwa Na LATRA kuendelea kutoa huduma Kwa sharti la kuingia na kutoka wapitie stendi Magufuli.

– Aagiza Manispaa ya Ubungo kukaa Na wamiliki wa stendi binafsi kuona njia bora kukusanya mapato.

Na: James lyatuu, DAR ES SALAAM 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametangaza kuondoa katazo lililokuwa likizuia Mabasi yaendayo mikoani na nje ya Nchi kutoruhusiwa kupakia abiria au kushusha katika Vituo binafsi na badala yake ameruhusu utaratibu huo kuendelea Kwa sharti la kila basi kuingia ndani ya Kituo kikuu Cha Mabasi Cha Magufuli.

RC Makalla ametoa maamuzi hayo wakati wa kikao Cha pamoja baina ya LATRA, Wamiliki wa Stendi binafsi na Halmashauri ya Ubungo na kubaini pasipokuwa na shaka kuwa Waliotengeneza Vituo binafsi walifuata taratibu na kupatiwa Vibali na LATRA Baada ya kukidhi vigezo.

Miongoni mwa vigezo vilivyotolewa na LATRA ili kuruhusiwa kuanzisha Stendi binafsi ni pamoja na uwepo wa Vyoo, Sehemu ya mapumzimo kwa abiria, viburudisho Na sehemu ya maegesho.

Kutokana na Hilo RC Makalla ameridhia Vituo binafsi 5 vilivyohakikiwa kuendelea kutoa huduma na kufungua milango kwa wamiliki wengine wanaohitaji kuwa na Vituo binafsi kushirikiana na LATRA ili wapatiwe vigezo vinavyohitajika ambapo wamepewa Mamlaka ya kufuta au kutoa leseni.

Aidha RC Makalla ameagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukaa kikao Mara moja na wamiliki wa Stendi binafsi ili kuona njia Bora ya ukusanyaji wa mapato.

Previous articleKINANA ATUA KIGOMA KWA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA
Next articleHUDUMA JUMUISHI ZA TIBA ASILI NA TIBA ZA KISASA KUANZA KUTOLEWA NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here