Home BUSINESS RC GEITA, 600 KUSHIRIKI MAONESHO YA MADINI 2022.

RC GEITA, 600 KUSHIRIKI MAONESHO YA MADINI 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela

Katibu tawala Mkoa wa Geita prof. Godius Kahyarara.

Na. Costantine James, Geita.

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Geita na Tanzania kwa ujmla kujitokeza kwa wingi katika maonesho ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayotarajiwa kufanyika mkaoani Geita kuanzia septemba 27 hadi oktoba 8, 2022 kwa lengo la kuja kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa katika uchimbaji wa madini.

Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Shigela amesema lengo kubwa la maonesho hayo ni kutoa elimu ya uchimbaji madini pamoja na biashara ya madini kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita pamoja maeneo mengine hii ni kutokana na maonesho hayo kuwakutanisha washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Shigela amesema washiriki zaidi ya 600 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki maonyesho hayo ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Geita kuanzia septemba 27 hadi oktoba 8, 2022.

Mhe, Shigela amesema mpaka sasa washiriki sita kutoka nchi sita ikiwemo China na India wamethibitisha kushiriki wao kwenye maonyesho hayo yanayotarajiwa kuwakutanisha wachimbaji wadogo, wakati na wakubwa kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.

Amesema kupitia maonesho hayo itakuwa ni njia moja wapo ya kujifunza teknolojia mpya hasa za uchimbaji wa madini kutoka kwa watalaamu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Shigela Amesema maonyesho haya ni muhimu mkubwa kufanyika katika mkoa wa Geita kutokana na Mkoa huo kuoongoza kwa uchimbaji wa madini hapa nchini na ni mkoa unaochangia mapato makubwa kwenye sekta ya madini.

“Maonyesho haya yanafanyika kila mwaka na kwa mwaka huu yatakuwa ya Kitaifa na Kimataifa washiriki zaidi ya 600 wakiwemo 12 kutoka nchi mbalimbali wamethibitisha kushiriki na watakuja kuonyesha teknolojia ya uchimbaji wa madini” amesema Shigela.

Shigela amesema maonyesho hayo mbali na kuwakutanisha wachimbaji wadogo,wakubwa na wafanyabiashara wa madini pia itakuwa ni fursa kwa mkoa huo kupata wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kufika Geita na kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika mkoa wa Geita.

Kwa upande wake Katibu tawala wa mkoa wa Geita professa Godius Kahyarara amesema maonyesho hayo ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya “Madini na fursa za uchumi ajira kwa maendeleo endelevu”.

Professa Kahyarara amesema mkoa huo unawachimbaji wadogo wengi wanaozalisha tani 5.8 kwa mwaka kutokana na matumizi ya teknolojia duni hivyo kupitia maonesho haya yatasaidia kutoa elimu juu ya matumizi ya njia za kisasa katika uchenjuaji hali itakayosaidia kuwezesha kuzalisha zaidi ya tani 20 hadi 25 kwa mwaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here