Home LOCAL RADI YAUA NG’OMBE 12 GEITA

RADI YAUA NG’OMBE 12 GEITA

Ng’ombe wapatao 12 wamekufa baada ya kupigwa na radi katika kijiji cha Mwingilo kata ya Ikunguigazi wilayani Mbogwe Mkoani Geita Wakati Ng’ombe hao wakiwa wanatoka malishoni majira ya mchana.

Tukio hilo limetokea wakati mvua ikinyesha ambapo kundi la Ng’ombe 15 wakiwa chini ya mti Baada ya radi kupiga ndipo ikapelekea ng’ombe 12 kuf, diwani wa kata ya Ikunguigazi Lutandula Poul Kazimoto amewataka wakazi wa kijiji hicho kutohusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio wamesema walisikia muungurumo mkali wakati mvua ikinyesha na ilipokata ndipo wakaona ng’ombe hao 12 wamekufa.0

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here