Meneja GCLA Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Musa Kuzumila (aliyesimama), akitoa mada kuhusu majukumu yanayotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, majukumu hayo yakiwemo matumizi salama ya kemikali katika uchimbaji, uchakataji na usafishaji wa madini.
Wakemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakitoa elimu kwa wateja waliotembelela banda la Mamlaka katika Maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini 2022, mkoani Geita.